Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2023


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema uwepo wa kifaa cha kupima uwepo na umbali   wa Madini Chini ya ardhi kilichonunuliwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, kitawasaidia Wachimbaji Madini kuchimba kwa tija na kupata faida.

Mhe. Senyamule amebainisha hayo leo Novemba 24/2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Jengo la Mkapa ambapo amefanya kikao kazi cha kusikiliza na kutatua kero mbalimbali za wafanyabiara wakubwa na wa kati wa Mkoa huo.

"Serikali Imenunua Mashine za kupima mkondo wa Madini ili kuwaondolea adha wachimbaji ili kujua kiwango na umbali ambao wachimbaji watakumbana nao hadi kuyafikia Madini yalipo na wataepukana na uchimbaji wa kubashiri hali ambayo itawaondolea kadhia ya kupoteza muda na nguvu walizotumia katika kuchimba eneo lisilo na Madini" Mhe. Senyamule

Aidha Mhe. Senyamule ametoa wito kwa wafanyabiashara kujenga hoteli zenye hadhi ya nyota tano ili kufungua fursa za kujiongezea vipato vyao.

"Nitoe wito kwenu kuwekeza katika Hoteli kubwa zenye hadhi ya nyota tano ili tuweze kupokea wageni wa kimataifa watakaokuja kufanya mikutano, makongamano na Michezo kutoka mataifa mbalimbali kwa sababu moja ya kigezo kinachokwamisha kufanyika kwa shughuli hizo kwenye Jiji letu ni ukosefu wa Hoteli zenye hadhi hizo", ametoa wito Mhe. Senyamule.

Hata hivyo, Mhe. Senyamule ameviainisha vyanzo mbalimbali vya mapato ambavyo Mkoa umejiwekea mkakati katika kuhakikisha vinauingizia mapato ya kutosha ambavyo ni Kilimo, Utalii, Viwanda, Madini pamoja na kuufanya Mji wa Dodoma kuwa Mji wa kimkakati (logistics hub).
Posted by MROKI On Saturday, November 25, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo