Nafasi Ya Matangazo

November 25, 2023

 







Mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary Chatanda, amesema Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameokoa maisha ya watoto njiti kwa kuongeza wodi ya Mama na Mtoto kwenye Hospitali ya Wilaya ya Bahi.

Ameyasema hayo leo 24 Novemba 2023 katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi na kuongea na wanachi Katika Halmashauri ya Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma.

“Hatuna budi kumshukuru Rais wetu Mama Samia kwa kuleta wodi yingi za Mama na Mtoto na kuokoa maisha na vifo vya watoto njiti kwani maisha yao yalikuwa hatarini.

“ lakini tunaona wananchi wanavyofurahia huduma zinazoletwa kwao kwani ni bora na sahihi kwa watoto” Amesema Chatanda.

Pia Chatanda, amefanya ziara ya kukagua miradi inayotekelezwa na ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika Nyumba ya Katibu wa UWT WIlaya ya Bahi yenye thamani ya Shilingi 7,900,000 Hospitali ya Wilaya yenye thamani ya shilingi Bilioni 3.2, na Shule Mpya ya Sekondari ya Chali yenye thamani ya shilingi Milioni 544 na kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua 

Vilevile, kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Bahi Mhe. Godwin Gondwe, amesema makusanyo ya ndani katika Halmashauri yake yamefikia  zaidi ya Bilioni 1.3 na kwa ujumla ambapo bajeti ambayo mpaka sasa Halmashauri imepokea fedha kutoka Serikali Kuu kiasi cha shilingi Bilioni 29.

“Mapato yameongezwa kwa kipindi hiki cha Uongozi wa Dkt. Samia Suluhu Hassan hadi kufikia asilimia 54 na yanasaidia shughuli za Wilaya ya Bahi huku asilimia 20 zikisaidia maendeleo na asilimia 80 zikitumika kwa matumizi mengine ya kawaida ya Halmashauri” Amesema Gondwe.
Posted by MROKI On Saturday, November 25, 2023 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo