Nafasi Ya Matangazo

October 26, 2024





Waziri Mkuu Kassim Majaliwa leo Oktoba 26, 2024 amekabidhi magari mapya 10 ikiwa ni ishara ya kukabidhi magari 88 yaliyonunuliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU) ambayo yatasambazwa mikoani kwa lengo la kuongeza tija na kuboresha utendaji kazi wa Taasisi hiyo.

Akitoa taarifa ya magari hayo, Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Crispin Chalamila amemweleza Waziri Mkuu kuwa katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan madarakani, TAKUKURU imepatiwa jumla ya Shilingi bilioni 30 za kununulia magari 195 ambapo 88 yameshanunuliwa.

“Mchakatio wa kununua magari 107 yaliyobakia unaendelea na tunatarajia kuyapata hivi karibuni, tunaahidi kutatunza magari haya ili kuongeza tija katika utendaji wetu” Amesema  Bw. Crispin.

Waziri Mkuu amekabidhi magari hayo wakati anafunga mafunzo ya awali ya uchunguzi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (TAKUKURU), hafla hiyo inafanyika kwenye Shule ya Polisi Tanzania, Moshi mkoani Kilimanjaro.
Posted by MROKI On Saturday, October 26, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo