WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, CPA. Hosea Kashimba, mara baada ya kuzunguzma na wastaafu watarajiwa
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na wastaafu watarjiwa jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2023.
*************
Na K-Vis Blog/Khalfan Said,
Dar Es Salaam.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amefungua semina elekezi kwa Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2023.
Akizungumza na wastaafu hao
kutoka mkoa wa Dar es Salaam, Profesa Ndalichako aliipongeza PSSSF kwa kuandaa
semina hiyo iliyobeba kauli mbiu isemayo “Wekeza Mafao yako Sehemu Salama kwa
Uhakika wa Ukwasi”.
Alisema lengo la semina hiyo
ni kuwajengea wastaafu wake watarajiwa uelewa na ufahamu juu ya umuhimu wa
kufanya maamuzi sahihi ya kukuza vipato vyao baada ya kustaafu ili kuleta tija
na uendelevu wa kipato.
“Usia wangu kwenu ni kuyatumia
vyema madini ya elimu mtakayoyapata hapa kwa kushikilia mambo makuu matatu nayo
ni kuwa na mtazamo chanya, kuweka mipango makini na kutimiza ndoto binafsi
baada ya kustaafu.” Alisema Profesa Ndalichako.
Alisema kustaafu ni wajibu kwa
kila mtumishi hivyo hakuna budi kuendeleza maisha mazuri hata baada ya
kustaafu.
Alisema ni vema mtumishi
akatambua kuwa safari ya kustaafu inaanza pale anapoanza ajira, hivyo ni muhimu
kujiandaa kimipango na kifedha ili kufurahia maisha ya uhuru lakini umakini
katika usimamizi wa fedha.
“Matumizi ya busara ya fedha
baada kustaafu ni muhimu zaidi kwani kwa kiasi kipato kinapungua na nguvu za
kufanya kazi zinaenda zikipungua siku hadi siku,” aliasa.
Awali Mkurugenzi Mkuu wa
PSSSF, CPA. Hosea Kashimba alisema PSSSF inatarajia kuwa na wastaafu 11,000
katika kipindi cha mwaka wa fedha 2023/2024.
Alisema Wastaafu watapatiwa
mafunzo ya elimu ya uwekezaji katika masoko ya fedha, taarifa za nyaraka na
utaratibu wa kufuata wakati wa kustaafu, kujiandaa kisakolojia baada ya kutoka
kwenye utumishi, umuhimu wa kutunza mazingira tunayoishi kutokana na mabadiliko
ya tabia ya nchi, na uhalifu wa kimtandao ambao unawaathiri wastaafu wengi.
“Mfuko katika kutambua na
kuunga mkono juhudi za Serikali katika kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi,
una mpango wa kutoa mche mmoja wa mti kwa kila mstaafu wa PSSSF.
“Mpaka sasa tuna wanachama
739,000 na lengo hapa ni kila mmoja aweze kupanda na kuutunza mche
tutakaompatia pindi atakapofikia wakati w akustaafu.”Alifafanua CPA. Kashimba.
Semina kama hii ilifanyika
mwaka 2021 kwa wastaafu watarijiwa 3700 bara na visiwani na mwaka huu pia elimu
itawafikia wastaafu kwenye mikoa ya Tanzania Bara na Visiwani, alisema CPA.
Kashimba.
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, amefungua semina elekezi kwa Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) jijini Dar es Salaam Septemba 11, 2023.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu), Mhe. Profesa Joyce Ndalichako, akizungumza na wastaafu watarjiwa jijini Dar es Salaam, Septemba 11, 2023. Kulia ni CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu, PSSSF.
Sehemu ya washiriki wa semina hiyo, wakiwemo wastaafu na wawezshaji (watoa mada).
Semina ikiendelea
CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, akizungumza na wastaafu watarajiwa
CPA. Hosea Kashimba, Mkurugenzi Mkuu, PSSSF, akizungumza na wastaafu watarajiwa
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi.
Baadhi ya watendaji wa Mfuko.
Meneja Uhusiano na Elimu kwa Wanachama, Bw. James Mlowe, akiongoza semina hiyo.
Baadhi ya watendaji wa Mfuko.
Baadhi ya watendaji wa Mfuko.
Mkurugenzi wa Uendeshaji PSSSF, Bw. Mbaruku Magawa, akizungumza mwanzoni mwa semina hiyo.
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi
Baadhi ya washiriki wa semina wakifuatilia hotuba ya mhgeni rasmi
Mmoja wa wastaafu akizunhguzma









0 comments:
Post a Comment