Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, (wa Pili kutoka kulia) akiwasha umeme katika moja ya nyumba katika Kijiji cha Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera ikiwa ni ishara ya kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, na viongozi wqengine mbalimbali wakikata utepe kuashiria uwashaji katika Kijiji cha Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera ikiwa ni ishara ya kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho.
Na Teresia Mhagama na Godfrey Lulinga
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, na viongozi wqengine mbalimbali wakikata utepe kuashiria uwashaji katika Kijiji cha Nyantakara wilayani Biharamulo mkoani Kagera ikiwa ni ishara ya kuwasha umeme kwenye Kijiji hicho.
Na Teresia Mhagama na Godfrey Lulinga
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, leo ameanza ziara ya
kikazi katika Mkoa wa Kagera ambapo katika siku ya kwanza ya ziara yake
amewasha umeme katika Kijiji cha Mubaba na Nyantakara vilivyopo wilayani
Biharamulo.
Akizungumza na wananchi pamoja na viongozi wa Serikali na wakandarasi wa umeme
vijijini, Dkt.Biteko ameagiza kuwa, sehemu zinazotoa huduma za kijamii kama vile
shule, visima vya maji na vituo vya afya
zipewe kipaumbele katika kupelekewa umeme ili wananchi waweze kupata huduma
bora.
" Haileti maana umeme kufika katika eneo fulani kama watoto wanasoma
gizani, haileti maana umeme kufika hapa halafu kina mama wanajifungulia gizani,
wala haina maana umeme kufika hapa wakati kuna vyanzo vya maji na tunashindwa kuwapelekea maji watu
wetu, ndio mana Rais wetu anataka mfikiwe na umeme ili usaidie kuboresha
huduma na kuchagiza shughuli za uchumi ." Amesema Dkt.Biteko
Dkt.Biteko ametoa wito kwa wananchi kulinda miundombinu ya umeme na wawakemee
watu wanaoiba miundombinu ya umeme ikiwemo nguzo, mafuta ya transfoma kwani
wanarudisha nyuma jitihada za kuwafikishia umeme wa uhakika wananchi.
Kuhusu wakandarasi wanaosimamia miradi ya umeme amesema kuwa, wahakikishe
wanafanya kazi kadri ya mikataba inavyoelekeza na kwamba kama kuna changamoto
zozote wazieleze kwa viongozi, lakini REA wakiona kuna mkandarasi ambaye
hafanyi kazi kama inavyotakiwa, mkandarasi huyo aondolewe na awekwe mwenye
uwezo.
Katika hatua nyingine, Dkt.Biteko amesema kuwa atasilimamia ipasavyo agizo la
Rais, Dkt.Samia Suluhu Hassan la kudhibiti changamoto ya kukatika mara kwa mara
kwa umeme ndani ya kipindi cha miezi sita.
" Agizo hili la Mhe.Rais tutalisimamia na kuhakikisha shida hii tunayoiona
ndani ya kipindi cha miezi tunaipunguza kwa kiasi kikubwa ili watanzania wapate
umeme wa uhakika."Amesema Biteko.
Kuhusu nishati safi ya kupikia amesema kuwa, Serikali inakuja na mpango
utakaowezesha wananchi kupunguza matumizi ya kuni na mkaa wa asili ambao una
athari kwa afya na kuleta nishati safi
ambapo REA inakuja na mpango unaojumuisha kugawa mitungi ya gesi kwa wananchi kwani lengo la Serikali ni kuhama kutoka nishati isiyo safi na kwenda
kwenye nishati safi.
Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt.Doto Biteko, akizungumza
na wananchi katika Kijiji cha Mubaba
wilayani Biharamulo mkoani Kagera wakati alipofika kuwasha umeme kwenye Kijiji
hicho.



.jpg)
.jpg)
.jpg)



0 comments:
Post a Comment