Naibu Waziri ambaye ana ziara ya siku tatu katika Mkoa huo alikuwaelekeza Watumishi wa Umma kujikita katika kuhakikisha wanazingatia na kutafsiri maono ya Rais Samia Suluhu Hassan pale aliwahimiza kuwe na Utumishi wenye kuleta tija, mbora, ulio kimkakati unaolenga kuwatumikia Wateja ambao ni wananchi.
Akizungumza na watumishi, Ndg. Naibu Waziri aliwaasa kuwa wabunifu na wenye mikakati ili kufikia malengo.
Pia katika tukio jengine,Naibu waziri Ndg. Kikwete amewaondoa kwenye Uratibu wa mpango wa TASAF waratibu wa Mkoa na Wale wa Wilaya kwa kile alichokiita kushindwa kufikia malengo ya kuwahudumia wananchi wangonge ambao wanahitaji sana huduma hii katika muda.











0 comments:
Post a Comment