Mkuu wa
kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga
akiongea wakati wa hafla ya kupokea vifaa vya uhamasishaji katika Wiki ya Nenda
kwa Usalama barabarani kutoka kampuni ya TBL Group,katikati ni Afisa Mawasiliano
wa kampuni hiyo,Amanda Walter na kushoto ni Mkurugenzi wa huduma za Zahanati
Mwendo,Rosemary Mwakitwange.
Afisa
Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter,akimkabidhi vifaa Mkuu wa
kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda Mohamed Mpinga wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam
Afisa
Mawasiliano wa kampuni hiyo,Amanda Walter,akiongea wakati wa hafla hiyo
iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
*****************
KATIKA
jitihada za kutokomeza ajali za barabarani nchini,kampuni ya TBL Group leo
imetoa vifaa vya uhamasishaji wa usalama katika wiki ya Nenda kwa
Usalama barabarani vilevile imekuja na huduma mpya ya kupima afya za
madereva ya zahanati inayotembea ‘Zahanati Mwendo’.
Akiongea
wakati wa hafla ya kukabidhi vifaa hivyo,Afisa Mawasiliano wa TBL Group,Amanda
Walter,alisema kuwa msaada huu ni mwendelezo wa kampuni kushiriki katika
kampeni za Usalama barabarani.
“TBL
Group ikiwa ni kampuni inayotengeneza vinywaji vyenye kilevi kwa muda mrefu
tumekuwa tukifanya kazi na serikali kupitia Jeshi la polisi katika kampeni za
kuhamasisha usalama barabarani lengo kubwa likiwa ni kutokomeza matukio ya
ajali nchini kupitia kampeni yetu ya usalama na Unywaji wa Kistaarabu”.Alisema
Amanda.
Alivitaja
vifaa vya uhamasishaji usalama katika Wiki ya Nenda na Usalama Barabarani kuwa
ni Stika 1,000,Tisheti 1000 na kofia 500 na imewezesha upimaji wa afya za
madereva kupitia Zahanati Mwendo “Huduma hii ni gari maalumu lenye vifaa vya
kupima afya za madereva na wataalamu wa afya na litakuwa linazunguka sehemu
mbalimbali nchini kwa ajili ya kupima afya za madereva na kuwapatia matibabu na
huduma hii itakuwa inapatikana bure kuanzia sasa hadi mwanzoni mwa mwezi ujao
na tutaendelea kufanya kampeni zaidi”.Alisema.
Kwa
upande wake Mkuu wa kikosi cha Usalama Barabarani wa Jeshi la Polisi,Kamanda
Mohamed Mpinga ,kwa niaba ya serikali aliishukuru TBL Group na wadau
wengine ambao wanashirikiana na jeshi hilo kufanikisha kampeni za usalama
barabarani.
Alisema
bado kuna matukio mengi ya ajali nchini ambazo zinasababisha vifo vya watu
wengi na kuleta hasara nyingi hivyo kunatakiwa jitihada za pamoja kufanya
kampeni ya kuzipunguza ikiwezekana hata kuzimaliza kabisa.
“Mwaka
huu TBL Group wamekuja na huduma ya kupima afya za madereva kupitia Zahanati
inayotembea ambayo ni ya aina yake nchini hivyo natoa wito kwa madereva wote
watakapoona gari hili maalumu litakalozunguka sehemu mbalimbali wajitokeze
kupima afya zao na kutakuwepo na vipimo vya macho,shinikizo la damu ,sukari na
vinginevyo tena vinatolewa bure”.Alisema Kamanda Mpinga.
Wiki ya
Usalama barabarani itafikia kilele wiki ijayo ambapo itafanyika kitaifa mkoani
Geita.
0 comments:
Post a Comment