Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh.
Aggrey Mwanri, akitoa soma la fursa kwa baadhi ya Wananchi wake
waliyojitokeza ndani ya Ukumi wa Chuo cha Uwaziri mjini Tabora mapema leo.
Msanii wa Muziki wa Kizazi
Kipya Nikki wa Pili akiwafungua wakazi wa Tabora kwa kuwaonyesha fursa
wanazopaswa kuzitumia ili waweze kusukuma mbele maendeleo ya mkoa huo.
Msanii wa Muziki wa Kughani
Mashairi, Mrisho Mpoto akiwa amenyanyua mikono juu wakati akiwapa mbinu za mafanikio
wakazi wa Tabora.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Mh. Aggrey Mwanri (wa nne kutoka kushoto), akiwa
kwenye picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wanasemina hiyo.
Mkurugenzi wa Vipindi na
Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mtahaba (katikati), akiongea jambo mbele
ya Mkuu wa Mkoa huo wakati akitoa somo la Fursa.
Afisa Masoko wa kanda ya kati
wa NMB, Josephine Kulwa akiwapatia fursa wakazi wa Tabora namna wanavyoweza
kufaidika na fursa mbalimbali kwa kujiunga na baadhi ya huduma zitolewazo na
benki hiyo. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
MKUU wa Mkoa wa Tabora MH.
Aggrey D.J Mwanri mapema leo alijikuta akitoa ya moyoni kwa kuisifia kamati na
uongozi mzima uliyoandaa tamasha la Fiesta 2016 kwa kuwapelekea Darasa la
Fursa.
Akizungumza ndani ya Ukumbi wa
chuo cha Uwaziri mjini Tabora wakati wa semina hiyo Mkuu wa Mkoa huo Mh. Aggery
Mwanri alisema kuwa, amefurahishwa sana na uongozi mzima wa Fiesta kwa
kuwawezesha wakazi wa mji huo kuwaonyesha namna ya kupambana kimaisha kwa kutumia
rasilimali zilizopo mkoa hapo.
“Napenda kutumia muda huu
kutoa pongezi zangu za dhati kwa waandaaji wa Tamasha la Fiesta hasa kupitia
darasa hili la Fursa ambalo naamini wazi kabisa kila mmoja wetu aliyehudhulia
hapa ataweza kujifunza na kuvuna mbinu mbadala za kujikwamua kimaisha na
kuufanya Mkoa wetu wa Tabora kuongeza uajibikaji,”
Pia Mh. Mwanra aliwaomba
wananchi wa mkoa huo kutumia fursa ya buruda zitakazo endelea usiku wa leo
katika Uwanja wa Ali Hassani Mwinyi kwa kusitarehe na kuangalia vitu vya msingi
vye kuwaongezea kipato zaidi.
Semini hiyo iliyokuwa
ikiongozwa na Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge
Mutahaba ilionekana kuchangamka vilivyo na kuwafanya baadhi ya wahudhuliaji
wakiwemo wanafunzi wa Chuo hicho kuomba darasa hilo liwe linawafikia mara kwa
mara mjini hapo.
0 comments:
Post a Comment