Nafasi Ya Matangazo

December 10, 2025

Tungependa tena kuendelea kutoa taarifa ya mwendelezo wa hali ya usalama hapa nchini kuanzia saa 12 asubuhi ya leo ya tarehe 10.12.2025 hadi mchana huu.

Hali ya usalama ni shwari na shughuli za kiuchumi na kijamii zinaendelea kama kawaida nchi nzima baada ya mapumziko ya jana tarehe 9.12.2025 ya sherehe za sikukuu ya Uhuru wa Taifa letu.

Jeshi la Polisi kwa ushirikiano na Vyombo vingine vya ulinzi na usalama vitaendelea kushirikiana na nyinyi wananchi kuhakikisha amani na usalama unaendelea kuimarika hapa nchini ili hata wale wachache wenye hofu waweze kutoka waendelee na shughuli zao za kila siku za kujitafutia riziki na kupata huduma za kijamii wanazo hitaji.

Aidha, tuna washukuru na kuwapongeza wananchi wote kwa nafasi zao kwa namna wanavyoendelea kuwakataa na kuwapuuza wale wanaohamasisha na kuchochea vurugu na ukiukwaji wa Sheria za nchi kupitia mitandao ya kijamii na njia zingine.

Aidha, tuna toa rai kwa kila mmoja wetu tuendelee kuungana kwa pamoja kulinda na kuimarisha amani na usalama wa Taifa letu ili liendelee kuwa sehemu salama ya kuishi kwa vizazi vya sasa na vitakavyo kuja. 


Posted by MROKI On Wednesday, December 10, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo