Nafasi Ya Matangazo

September 22, 2016

 Kikosi cha mauzo na usambazaji kutoka DARBREW katika picha ya pamoja wakati  wa uzinduzi wa kampeni ya Five Star
 Baadhi ya wafanyakazi wakifurahia uzinduzi wa kampeni ya 5 Star ambayo inaendelea kuwafikia wananchi mitaani
Kampeni ya uhamasishaji utumiaji wa bia ya asili ya Chibuku Super inayojulikana kama ‘Five Star’ inayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam na sehemu mbalimbali kinapopatikana kinywaji hiki inazidi kupamba moto na inaendelea kuwezesha wananchi wengi kuelewa ubora wake na kwa jinsi gani kinaleta burudani sambamba na kupunguza gharama za maisha.
 
Jina la Five Star au Nyota Tano kwa Kiswahili katika kampeni hii ambapo kila nyota inaeleza hali halisia wa bia hii ya asili na ubora wake katika kuitumia.
 
 Nyota ya kwanza inaelezea kuwa Bia ya asili ya Chibuku ni Bia ya asili ya Kiafrika kutokana na jinsi inavyokubalika katika nchi mbalimbali za Afrika  kwa kutumiwa na wengi kama kiburudisho baada ya saa za kazi.
 
Nyota ya pili inaelezea vionjo vyenye kiwango cha juu vya bia ya Chibuku vinavyotokana na mchanganyiko wa malighafi za nafaka zinazotumika kutengenezea kinywaji hiki
 
Nyota ya tatu inaelezea radha inayoridhisha ya bia ya Chibuku   ambayo inapendeza mdomoni na kuleta raha na burudani ya aina yake.
 
Nyota ya nne inaelezea ubora wa hali ya juu wa bia ya asili ya Chibuku  kutokana na kutengenezwa kitaalamu na kuwa na viwango vinavyotakiwa vya ubora usioleta madhara kwa mtumiaji
 
Nyota ya tano inaelezea kuwa bia ya Chibuku ni kwa ajili yetu sote kutokana na ubora wake inaweza kutumiwa na watu wenye mitindo ya maisha ya aina mbalimbali pia inapatikana kwenye chupa zenye ujazo wa aina mbalimbali,hali ambayo inawezesha mtumiaji kukipata kinywaji hiki kulingana na mfuko wake ulivyo.
 
Kampeni  ya Five Stars inaendelea kufanyika kwenye vilabu  na sehemu nyingi inapouzwa bia ya Chibuku Super na inazidi kuwafikia wengi na watumiaji wake kuongezeka , wengi mbali na kuvutiwa na radha nzuri ya bia hii  ya asili wanavutiwa kwa jinsi ilivyofungwa na inavyowafikia watumiaji ikiwa katika mazingira ya usafi na wengi wanakiri  kuwa Chibuku ni bia  ya asili ya kitanzania inayolinda  afya za watumiaji wake na kurahisisha maisha
Posted by MROKI On Thursday, September 22, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo