Arusha, 08 Januari, 2025
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ina jukumu la kukadiria, kukusanya na
kuhasibu mapato ya serikali kuu. Katika hali ya kutambua mchango mkubwa wa
walipakodi, TRA imekuwa na utamaduni wa kuwashukuru na kuwapongeza walipakodi
na wadau wetu kutokana na mchango wao mkubwa wa kulipa kodi au kurahisisha
ulipaji wa kodi.
TRA tumetenga tarehe 23 Januari, 2025 kuwa siku maalumu ya kutambua na kutoa
shukrani na tuzo kwa Mlipakodi waliotekeleza wajibu wao wa kisheria kwa hiari
kwa mwaka 2023/2024.
Lengo la kutoa tuzo hizi ni kutambua juhudi za walipakodi na kuunga
mkono taasisi/watu binafsi waliowezesha TRA kukusanya kodi kwa urahisi.
Walipakodi watakaotunukiwa ni wale walioonesha mwitikio wa hali ya juu kwa
hiari, mchango mkubwa katika ukusanyaji wa mapato, na wasio na rekodi yoyote ya
udanganyifu au ukwepaji wa kodi katika kipindi husika. TRA inashirikiana kwa
karibu na wadau mbalimbali kufanikisha malengo yake, na kwa sababu hiyo, wadau
wenye kiwango cha juu zaidi cha ushirikiano watapewa tuzo pia.
Mwaka huu, jumla ya walipakodi na wadau 1228 watatunukiwa vikombe, ngao,
na vyeti kama ishara ya kutambua mchango wao katika kujenga taifa kupitia
ulipaji wa kodi kwa hiari au kwa kusaidia TRA kwa njia moja au nyingine katika
ukusanyaji wa mapato. Ili kustahili kuchaguliwa kupata tuzo za Mlipakodi,
vigezo vifuatavyo ni vimezingatiwa:-
Walipakodi waliotimiza vigezo vilivyotajwa watazingatiwa, mradi kwamba
walipakodi hao hawajajihusisha na udanganyifu au ukwepaji wa kodi katika
kipindi husika.
Aidha, kutakuwepo na vipengele
vya washindi wa kitaifa kama vifuatavyo:-
1. Walipakodi waliofuata
sheria za kodi kwa hiari
2. Walipakodi waliolipa
kiasi cha kodi kikubwa kwenye ngazi ya wilaya au mkoa au kitaifa.
3.Walipakodi
waliowasilisha nyaraka sahihi za forodha na kwa wakati.
Wakati tunaadhimisha siku ya Shukrani kwa Mlipakodi Mamlaka ya Mapato
Tanzania inapenda kutoa wito kwa walipakodi wote kuendelea kulipa kodi stahiki
na kwa wakati. TRA pia inawahimiza wafanyabiashara wote kuendelea kutimiza
wajibu wao wa kutoa risiti halali kila
wanapouza, na mwananchi kuhakikisha wanadai risiti za EFD, kwani hiyo ndiyo
njia pekee inatuunganisha watanzania wote kulipa kodi ya Serikali.
“Pamoja
Tunajenga Taifa Letu”
I. Uzingatiaji wa sheria
za kodi kwa hiari.
II.Kulipa kiasi kikubwa
cha Kodi au Ushuru kwa mwaka wa fedha 2023/24.
III.Ulipaji kodi kwa hiari
katika kipindi cha mwaka husika 2023/2024.
IV. Uzingatiaji wa matumizi
ya mashine za VFD/EFD kwa usahihi.
V. Kuwasilisha ritani za
kodi au nyaraka za forodha kwa wakati na kwa usahihi.
VI. Kulipa kodi na ushuru wa
forodha kwa wakati na kwa usahihi.
VII.Kutohusika katika
ukwepaji wa kodi na shughuli za udanganyifu.
VIII.Kutoa ushirikiano kwa
TRA katika masuala ya kikodi pindi inapohitajika
IX.Kuboresha kiwango cha
utendaji kazi katika maeneo yote ya uendeshaji.
Richard
M. Kayombo
Mkurugenzi wa Elimu kwa Mlipakodi na
Mawasiliano
0 comments:
Post a Comment