Kikosi
cha mauzo na usambazaji kutoka DARBREW katika picha ya pamoja wakati wa uzinduzi wa kampeni ya Five Star
Baadhi
ya wafanyakazi wakifurahia uzinduzi wa kampeni ya 5 Star ambayo inaendelea
kuwafikia wananchi mitaani
Kampeni
ya uhamasishaji utumiaji wa bia ya asili ya Chibuku Super inayojulikana kama
‘Five Star’ inayoendelea kufanyika jijini Dar es Salaam na sehemu mbalimbali
kinapopatikana kinywaji hiki inazidi kupamba moto na inaendelea kuwezesha
wananchi wengi kuelewa ubora wake na kwa jinsi gani kinaleta burudani sambamba
na kupunguza gharama za maisha.
Jina
la Five Star au Nyota Tano kwa Kiswahili katika kampeni hii ambapo kila nyota
inaeleza hali halisia wa bia hii ya asili na ubora wake katika kuitumia.
Nyota ya kwanza inaelezea kuwa Bia ya asili ya
Chibuku ni Bia ya asili ya Kiafrika kutokana
na jinsi inavyokubalika katika nchi mbalimbali za Afrika kwa kutumiwa na wengi kama kiburudisho baada
ya saa za kazi.
Nyota
ya pili inaelezea vionjo vyenye kiwango
cha juu vya bia ya Chibuku vinavyotokana na mchanganyiko wa malighafi za
nafaka zinazotumika kutengenezea kinywaji hiki
Nyota
ya tatu inaelezea radha inayoridhisha
ya bia ya Chibuku ambayo inapendeza
mdomoni na kuleta raha na burudani ya aina yake.
Nyota
ya nne inaelezea ubora wa hali ya juu
wa bia ya asili ya Chibuku kutokana na
kutengenezwa kitaalamu na kuwa na viwango vinavyotakiwa vya ubora usioleta
madhara kwa mtumiaji
Nyota
ya tano inaelezea kuwa bia ya Chibuku ni kwa
ajili yetu sote kutokana na ubora wake inaweza kutumiwa na watu wenye
mitindo ya maisha ya aina mbalimbali pia inapatikana kwenye chupa zenye ujazo
wa aina mbalimbali,hali ambayo inawezesha mtumiaji kukipata kinywaji hiki
kulingana na mfuko wake ulivyo.
Kampeni ya Five Stars inaendelea kufanyika kwenye
vilabu na sehemu nyingi inapouzwa bia ya
Chibuku Super na inazidi kuwafikia wengi na watumiaji wake kuongezeka , wengi
mbali na kuvutiwa na radha nzuri ya bia hii
ya asili wanavutiwa kwa jinsi ilivyofungwa na inavyowafikia watumiaji
ikiwa katika mazingira ya usafi na wengi wanakiri kuwa Chibuku ni bia ya asili ya kitanzania inayolinda afya za watumiaji wake na kurahisisha maisha
No comments:
Post a Comment