Meneja
Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray
(kushoto) pamoja na wafanyakazi wa Tbl Group Kitengo cha
Mawasiliano, Zena Tenga , Irene Mutigazi na Abigail
Mutaboyerwa.wakimsikiliza kwa makini Mpishi Mkuu wa bia ,Benjamin Budigila (kushoto)
kuhusiana na uzalishaji wa bia.
Meneja
Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray
(kulia) akiangalia moja ya mtambo unaopitisha bia wakati
alipotembelea katika Kiwanda cha bia Ilala jijini Dar es Salaam
kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za ujazalishaji wa vinywaji
(Kushoto) anayeshuhudia ni mpishi Mkuu wa bia Benjamin Budigila.
Mpishi
Mkuu wa bia wa TBL Group,Benjamin Budigila (kushoto) akiwaonyesha moja ya
mtambo unaotumika kuzalisha bia , Maofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Zena Tenga ,(katikati )na msaidizi
wake Abigail Mutaboyerwa wakati walipotembelea kiwandani hapo Ilala
jijini Dar es Salaam katika ziara ya Afisa wa kampuni ya Trash back ya
Afrika Kusini.
Wafanyakazi
wa TBL Group kitengo cha Mawasiliano wakielekezwa na : Mpishi Mkuu wa bia
wa TBL Group,Benjamin Budigila (wapili kulia) mtambo wa uzalishaji wa bia
.Kulia ni Meneja Biashara na Maendeleo wa kamapuni ya Trash back ya Afrika
Kusini ,Andrew Murray. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.
MENEJA wa Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya nchini Afrika yuko nchini kwa ziara ya kikazi nchini ambapo amefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha TBL kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo amevutiwa na mkakati wa utunzaji wa mazingira unaofanywa na kampuni hiyo.
Trash back ni kampuni kubwa
nchini Afrika ambayo imekuwa ikijihusisha na usafi wa mazingira mijini hususani
kuzoa taka na kutoa ushauri wa jinsi ya kusaga taka na kuzibadilisha kwa
matumizi mbadala yenye kuleta manufaa kwa jamii.
TBL Group inao mkakati wa
utunzaji wa mazingira ili kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kutokana
na uzalishaji kwenye viwanda vyake na tayari inatekeleza mpango wa kusaga
takataka zinazozalishwa katika mchakato wa uzalishaji na kuhakikisha zinatumika
kwa matumizi mengineyo .
Kampuni pia imekuwa mstari
wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira ikiwemo
kupanda miti na inayo mikakati mbalimbali ya kuendesha miradi ya utunzaji wa
mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na katika kupambana na tatizo la
taka jijini Dar es Salaam imewaalika wataalamu wa mazingira kutoka Trash Back
ili watoe ushauri wa kusaga taka na tayari wamekutana na watendaji wa Manispaa
ya Ilala na kutembelea madampo ya taka yaliyopo wilayani Ilala.
0 comments:
Post a Comment