September 08, 2016

AFISA MWANDAMIZI WA TRASH BACK ATEMBELEA KIWANDA CHA TBL GROUP



Meneja Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray (kushoto)  pamoja na wafanyakazi wa Tbl Group Kitengo cha Mawasiliano,  Zena Tenga , Irene Mutigazi  na Abigail Mutaboyerwa.wakimsikiliza kwa makini Mpishi Mkuu wa bia ,Benjamin Budigila (kushoto) kuhusiana na uzalishaji wa bia.


Meneja Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray (kulia)  akiangalia moja ya mtambo unaopitisha bia wakati alipotembelea  katika Kiwanda cha bia  Ilala jijini Dar es Salaam  kwa ajili ya kujifunza shughuli mbalimbali za ujazalishaji wa vinywaji (Kushoto) anayeshuhudia ni mpishi Mkuu wa bia  Benjamin Budigila.


Mpishi Mkuu wa bia wa TBL Group,Benjamin Budigila (kushoto) akiwaonyesha moja ya mtambo unaotumika  kuzalisha bia ,  Maofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo,  Zena Tenga ,(katikati )na msaidizi wake  Abigail Mutaboyerwa wakati walipotembelea kiwandani hapo Ilala jijini Dar es Salaam  katika ziara ya Afisa wa kampuni ya Trash back ya Afrika Kusini.     


Wafanyakazi wa TBL Group kitengo cha Mawasiliano  wakielekezwa na : Mpishi Mkuu wa bia wa TBL Group,Benjamin Budigila (wapili kulia) mtambo wa uzalishaji wa bia .Kulia ni Meneja Biashara na Maendeleo wa kamapuni ya Trash back ya Afrika Kusini ,Andrew Murray. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI.

MENEJA wa Biashara na Maendeleo wa kampuni ya Trash back ya nchini Afrika yuko nchini kwa ziara ya kikazi nchini ambapo amefanya ziara ya kutembelea kiwanda cha TBL kilichopo jijini Dar es Salaam ambapo amevutiwa na mkakati wa utunzaji wa mazingira unaofanywa na kampuni hiyo.

Trash back ni kampuni kubwa nchini Afrika ambayo imekuwa ikijihusisha na usafi wa mazingira mijini hususani kuzoa taka na kutoa ushauri wa jinsi ya kusaga  taka na kuzibadilisha kwa matumizi mbadala yenye kuleta manufaa kwa jamii.

TBL Group inao mkakati wa utunzaji wa mazingira ili kupunguza athari za uharibifu wa mazingira kutokana na uzalishaji kwenye viwanda  vyake na tayari inatekeleza mpango wa kusaga takataka zinazozalishwa katika mchakato wa uzalishaji na kuhakikisha zinatumika kwa matumizi mengineyo .

Kampuni pia imekuwa mstari wa mbele kuunga mkono jitihada za serikali za utunzaji wa mazingira ikiwemo kupanda miti na inayo mikakati mbalimbali ya kuendesha miradi ya utunzaji wa mazingira kwa kushirikiana na wadau mbalimbali na katika kupambana na tatizo la taka jijini Dar es Salaam imewaalika wataalamu wa mazingira kutoka Trash Back ili watoe ushauri wa kusaga taka na tayari wamekutana na watendaji wa Manispaa ya Ilala na kutembelea madampo ya taka yaliyopo wilayani Ilala.

No comments:

Post a Comment