Nafasi Ya Matangazo

August 30, 2016



NA K-VIS MEDIA
SHIRIKA la Umeme Tanzania, (TANESCO), linapenda kuuarifu umma kuwa kutakuwepo na katizo la umeme KUANZIA Septemba 3, 2016 kwenye maeneo mengi ya jiji la Dar es Salaam kutokana na kazi kubwa ya kuboresha miundombinu ya umeme kwenye kituo kikubwa cha kupoza na kusambaza cha Msongo wa Kilovolti 132 cha Ubungo-Ilala.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Uhusiano ya Shirika hilo, Makao Makuu jijini Dar es Salaam leo Agosti 30, 2016, katizo hilo la umeme litaanza rasmi Septemba 3 na umeme utakuwa ukikatika kuanzia saa 2 asubuhi na kurejea saa 11 jioni kwa utaratibu na tarehe kama ifuatavyo; Septemba 3-4, Septemba 10-11, Septemba 17-18, na Septemba 24-25, 2016. 
Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoathirika na zoezi hilo kuwa ni pamoja na eneo lote la katikati ya jiji (City centre), Maeneoyote ya Upanga, maeneo yote ya Kariakoo, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Mbagala, Maeneo yote ya Buguruni, Maeneo yote ya Ilala, Maeneo yote ya Chang’ombe, Maeneo ya Temeke, Uwanja wa Taifa, Unilever, Makao Makuu ya Puma, Temesa, Jamana printers, Quality Plaza, Notco, Bima ya Afya, Bandari Gate pamoja na maeneo ya jirani.
Taarifa hiyo imefafanua kuwa ili jiji la Dar es Salaam lipate umeme ulio bora na wa uhakika, Shirika laUmeem Tanzania (TANESCO), limemruhusu mkandarasi, (TAKAOKA), kubadilisha vikombe na nyaya na kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa za njia mbili (Two-lines) za Msongo wa Kilovolti 132.
Kuboresha vituo vya kupoza na kusambaza umeme vya Ilala na Ubungo kwa kuweka nyaya zenye uwezo mkubwa zaidi.
Kubadilisha vifaa vya kupima umeme kwenye njia mbili (Two-lines) za Ubungo-Ilala.

Posted by MROKI On Tuesday, August 30, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo