October 15, 2015

RAIS KIKWETE AFUNGUA RASMI JENGO LA OFISI YA TAIFA YA UKAGUZI DODOMA

Rais  Jakaya Mrisho Kikwete, leo, tarehe 15 Oktoba, 2015, amelifungua rasmi jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa ufunguzi huo, Rais Kikwete ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa kujenga jengo zuri linaloakisi sifa na heshima ya utendaji wa Ofisi hiyo.

Kwa upande wake CAG, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuiwezesha ofisi yake na kuongeza uhuru wa ofisi hiyo kwa kuwawezesha kujenga majengo katika mikoa ya Singida, Morogoro na Kilimanjaro. 

Ufunguzi huo ulishuhudiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad, baadhi ya viongozi waandamizi na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kutoka Makao Makuu na Dodoma. Kwa upande wa Wizara ya Fedha walioshuhudia ni Waziri wa Fedha, Bibi Saada Mkuya na Katibu Mkuu wake, Dkt. Servacius Likwelile. Jengo hili limekusudiwa kuwa makao makuu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati alipofika kuzindua jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad wakifurahia baada ya kufungua kibao cha uzinduzi wa jengo hilo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) kwa pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (kulia) na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakikata utepe kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma. Kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kulia).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais  Jakaya Mrisho Kikwete (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma. Wengine pichani waliokaa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa (kushoto), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad (wapli kushoto). Wengine ni Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (wapili kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (kulia).

No comments:

Post a Comment