Rais Jakaya Mrisho Kikwete, leo,
tarehe 15 Oktoba, 2015, amelifungua rasmi jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi
mkoani Dodoma.
Akizungumza
wakati wa ufunguzi huo, Rais Kikwete ameipongeza Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi kwa
kujenga jengo zuri linaloakisi sifa na heshima ya utendaji wa Ofisi hiyo.
Kwa
upande wake CAG, aliishukuru Serikali ya Awamu ya Nne kwa kuiwezesha ofisi yake
na kuongeza uhuru wa ofisi hiyo kwa kuwawezesha kujenga majengo katika mikoa ya
Singida, Morogoro na Kilimanjaro.
Ufunguzi
huo ulishuhudiwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof.
Mussa Assad, baadhi ya viongozi waandamizi na watumishi wa Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi kutoka Makao Makuu na Dodoma. Kwa upande wa Wizara ya Fedha
walioshuhudia ni Waziri wa Fedha, Bibi Saada Mkuya na Katibu Mkuu wake, Dkt.
Servacius Likwelile. Jengo
hili limekusudiwa kuwa makao makuu ya Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia
baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi wakati alipofika kuzindua
jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa
Assad wakifurahia baada ya kufungua kibao
cha uzinduzi wa jengo hilo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) kwa
pamoja na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa
Assad (kulia) na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (kushoto) wakikata utepe
kuashiria ufunguzi rasmi wa Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati)
akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya
Taifa ya Ukaguzi, mkoani Dodoma. Kushoto ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu
za Serikali (CAG), Prof. Mussa Assad na Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya
(kulia).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati waliokaa)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi waandamizi wa Ofisi ya Taifa
ya Ukaguzi mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi,
mkoani Dodoma.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete (katikati waliokaa)
akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Taifa ya
Ukaguzi mara baada ya kulifungua rasmi Jengo la Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi,
mkoani Dodoma. Wengine pichani waliokaa ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa
(kushoto), Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Prof. Mussa
Assad (wapli kushoto). Wengine ni Waziri wa Fedha Mhe. Saada Mkuya (wapili
kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius Likwelile (kulia).
0 comments:
Post a Comment