October 15, 2015

WABUNIFU WA MAVAZI NCHINI WAKUSANYA NGUVU KWA PAMOJA KUHUBIRI JUU YA UMUHIMU WA AMANI

Mbunifu wa Mavazi nchini, Mustafa Hassanali akizungumza na  Waandishi wa Habari hawapo pichani juu ya umuhimu wa Amani hususani katika kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, Mwaka huu na kusisitiza onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe Oktoba  17 Mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon uliopo Eater Point Namanga, ambalo litakaloonyesha kazi za wa wabunifu mbalimbali kama Kiki Zimba pamoja na Martin Kadinda.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wakisikiliza kwa makini taarifa iliyokuwa inatolewa na Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika,Mstafa Hassanali juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25,Mwaka huu.
*****************
Na Bakari Issa
Wabunifu wa Mavazi nchini Tanzania, Mustafa Hassanali,Kiki Zimba pamoja na Martin Kadinda wameazimia kukusanya nguvu kwa pamoja ili kuhubiri juu ya umuhimu wa Amani hususan kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25,Mwaka huu.

Wabunifu hao wamekusanya nguvu kwa pamoja kwa kuwa na onyesho la mavazi litakalo fanyika tarehe 17 Octoba Mwaka huu katika ukumbi wa King Solomon uliopo Eater Point Namanga,ambalo litakalo onyesha kazi za ubunifu zilizofanywa na wabunifu hao watatu.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es Saalam,Mbunifu Mkongwe wa Mavazi Barani Afrika ,Mustafa Hassanali amesema kutokana na wimbo wetu wa Taifa “Hekima,Umoja na Amani,hizi ni Ngao zetu”kuna umuhimu kwa vijana kukuza na kulinda Uhuru,Amani na Utulivu wa nchi.

Kwa Upande wake,Martin Kadinda amesema Uchaguzi Mkuu ni wa muhimu sana,hivyo basi vijana wa Kitanzania wahakikishe wanapiga kura kwa Amani katika Uchaguzi Mkuu wa Octoba 25 na kukaa katikahali ya Utulivu kwa kufuatilia na kukubali matokeo yatakayotangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi(NEC) katika hali ya Amani.

No comments:

Post a Comment