Wanachama
wa Chama cha United Democratic Forum (UDF) wamemteua rasmi Mwenyekiti wa Chama
hicho na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Wycliffe Musalia Mudavadi kuwa mgombea
rasmi wa Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Urais unaotaraji kufanyika Mwezi
Machi mwaka huu.
Mudavadi
aliyezaliwa Sabatia, wilayani Vihiga mwaka 1960 endapo atashinda Kinyang’anyiro
hicho anaweza kuwa Rais wa nne wa Jamhuri ya Watu wa Kenya na kabla ya kuhamia
UDF alikuwa ni Kiongozi wa Juu wa chama cha ODM kinachoongozwa na Waziri Mkuu
wa Kenya, Raila Odinga.
Udavad
alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa jimbo la Sabnatia mwaka 1989
akitokea kambi ya Upinzani Bungeni baada ya kuchukua nafasi ya BABA YAKE Mzee Moses
Mudavad.
Mwaka
2002 Mudavad alikuwa ni Makamu wa Ras wa mwisho na ambaye alihudumu kwa
kipoindi kifupi kuliko Makamu wa Rais wote kipindi cha Utawala wa Rais Daniel
Arap Moi, na alichaguliwa ili ku;lifanya kabila la Luhya kuwa ndani ya chama
cha KANU.
Mudavadi alikuwa ni
Mgombea mwenza wakati Uhuru Kenyatta
akiwania Urais uchaguzi wa 2002.
Katika uchaguzi wa
mwaka 2007, Mudavadi pia alikuwa Mgombea Mwenza wa Raila Odinga kupitia chama
cha ODM, ambacho kilizaliwa kutoka muungano wa Vyama vya ODM-K na kuangushwa na
Rais wa sasa wa Kenya, Mwai Kibaki na baade kukubaliana kuanzisha serijkali ya
Mseto ambapo Odinga aliteuliwa kuwa Wazziri Mkuu na Mudavadi kuteuliwa kuwa
Naibu waziri Mkuu kutoka ODM na Uhuru Kenyatta akiwa Naibu Waziri Mkuu kutoka PNU
cha Kibaki.
Baada ya kuanza kwa
harakati za Uchaguzi 2012, na kubadilika kwa Katiba ya Chama cha ODM yakuwa
Mwenyekiti wa Chama ndio akaamua kujiengua na kuumngana na Uhuru Kenyatta na William Ruto na kuweka muungano wa vyama
vya UDF, URP na TNA na baadae Mudavadi akaondoka katika muungano huo baada ya
kukiukwa moja ya kanuni za Muungano juu ya mgombea Urais ambapo baadhi ya
wafuasi wa Kenyatta walitaka ndie agombee Urais kwa Umoja huo.
0 comments:
Post a Comment