January 04, 2013

UDF YAMTEUA MUSALIA MUDAVADI KUWANIA URAIS WA KENYA

Wanachama wa Chama cha United Democratic Forum (UDF) wamemteua rasmi Mwenyekiti wa Chama hicho na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya, Wycliffe Musalia Mudavadi kuwa mgombea rasmi wa Chama hicho katika Uchaguzi Mkuu wa Urais unaotaraji kufanyika Mwezi Machi mwaka huu.

Mudavadi aliyezaliwa Sabatia, wilayani Vihiga mwaka 1960 endapo atashinda Kinyang’anyiro hicho anaweza kuwa Rais wa nne wa Jamhuri ya Watu wa Kenya na kabla ya kuhamia UDF alikuwa ni Kiongozi wa Juu wa chama cha ODM kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga.

Udavad alichaguliwa kwa mara ya kwanza kuwa Mbunge wa jimbo la Sabnatia mwaka 1989 akitokea kambi ya Upinzani Bungeni baada ya kuchukua nafasi ya BABA YAKE Mzee Moses Mudavad.

Mwaka 2002 Mudavad alikuwa ni Makamu wa Ras wa mwisho na ambaye alihudumu kwa kipoindi kifupi kuliko Makamu wa Rais wote kipindi cha Utawala wa Rais Daniel Arap Moi, na alichaguliwa ili ku;lifanya kabila la Luhya kuwa ndani ya chama cha KANU.

Mudavadi alikuwa ni Mgombea mwenza wakati  Uhuru Kenyatta akiwania Urais uchaguzi wa 2002.

Katika uchaguzi wa mwaka 2007, Mudavadi pia alikuwa Mgombea Mwenza wa Raila Odinga kupitia chama cha ODM, ambacho kilizaliwa kutoka muungano wa Vyama vya ODM-K na kuangushwa na Rais wa sasa wa Kenya, Mwai Kibaki na baade kukubaliana kuanzisha serijkali ya Mseto ambapo Odinga aliteuliwa kuwa Wazziri Mkuu na Mudavadi kuteuliwa kuwa Naibu waziri Mkuu kutoka ODM na Uhuru Kenyatta akiwa Naibu Waziri Mkuu kutoka PNU cha Kibaki.

Baada ya kuanza kwa harakati za Uchaguzi 2012, na kubadilika kwa Katiba ya Chama cha ODM yakuwa Mwenyekiti wa Chama ndio akaamua kujiengua na kuumngana na Uhuru Kenyatta  na William Ruto na kuweka muungano wa vyama vya UDF, URP na TNA na baadae Mudavadi akaondoka katika muungano huo baada ya kukiukwa moja ya kanuni za Muungano juu ya mgombea Urais ambapo baadhi ya wafuasi wa Kenyatta walitaka ndie agombee Urais kwa Umoja huo.

No comments:

Post a Comment