Mama Tunu Pinda akiwa ni mmoja wa umoja wa wake wa viongozi mbalimbali wameamua kushiriki kuihamasisha jamii na wadau mbalimbali kuisaidia timu ya mpira ya wanawake ya Netboli (Taifa Queens ) kuhakikisha inafanikisha malengo yake na pia kuhakikisha maandalizi yote yanakwenda sawa.Pichani ni Mama Tunu Pinda akizungumza leo kwenye kipindi cha Powerbreakfast kupitia redio ya Clouds FM jijini Dar kuhusiana na mchakato mzima wa kuisadia Taifa Queens,kulia ni Paul James a.k.a PJ.
Taifa Queens kwa sasa iko kambini kwa ajili ya maandalizi ya mashidano ya Netiboli ya Kombe la Afrika,ambapo Tanzania kupitia CHANETA imepewa heshima ya kuandaa Mashindano ya Netiboli ya Kombe la Afrika ambayo yanatarajiwa kuanza Mei 8-12, mwaka huu. Mama Tunu Pinda aliweka bayana kuwa gharama za kuendesha mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 127.
Hivyo Mama Pinda amewaomba wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kufanya vyema kwenye michuano yake,aidha amewataka Wadau watakaokuwa na nia kuichangia timu hiyo basi watume michango yao kupitia namba ya simu 0779 000 808 (huduma ya Easy pesa),ambapo mtu ama kampuni anaweza kutuma kwenye namba hiyo kwa mitandano yote.
Hivyo Mama Pinda amewaomba wadau mbalimbali kuisaidia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kufanya vyema kwenye michuano yake,aidha amewataka Wadau watakaokuwa na nia kuichangia timu hiyo basi watume michango yao kupitia namba ya simu 0779 000 808 (huduma ya Easy pesa),ambapo mtu ama kampuni anaweza kutuma kwenye namba hiyo kwa mitandano yote.
Mama Pinda akipata maelezo mafupi kwenye studio ya Choice FM kutoka kwa mtangazaji Baby Kabae.
Mama Pinda akipata maelezo mafupi kwenye studio B ya Clouds FM namna inavyoweza kufanya kazi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Clouds Media Group ,Bw.Joseph Kusaga akimpa Mama Pinda zawadi ya jarida la burudani la Kitangoma linalochapishwa na kampuni bingwa ya burudani hapa nchini ya Prime Time Promotions Ltd.
Mama Pinda akimshangaa Bonge,mwenye anatabasamu tuuu...!
Mkuu wa Kitengo cha Habari Clouds FM/TV Dada Joyce Shebe akimkaribisha Mama Pinda Newsroom ya kituo hicho,mara baada ya kupata wasaa wa kutembelea pia vitengo mbalimbali vya kampuni hiyo
Mama Pinda akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Clouds Media Group na mie.
Mke wa waziri Mkuu,Mama Tunu Pinda (pili kulia) akiwa amepozi katika picha ya pamoja na Watangazaji wa kipindi cha Power breakfast kutoka Clouds FM mapema leo asubuhi,Mama Pinda alifika kwenye ofisi za redio hizo kwa ajili ya kuwahamasisha jamii mbalimbali kuisaidia timu ya Taifa Queens kwenye michuano yake inayotarajiwa kuanza hivi karibuni hapa jijini dar
0 comments:
Post a Comment