Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ramadhan Abdalla Shaaban,kuwa Waziri wa Ardhi.Makaazi,Maji na Nishati,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,kabla Shaaban,alikuwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Ali Juma Shamuhuna,kuwa Waziri wa Elimu na Mfunzo ya Amali,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,kabla Shamuhuna,alikuwa Waziri wa Ardhi,Makaazi Maji na Nishati.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Suleiman Othman Nyanga,kuwa Waziri wa Kilimo na Maliasili,katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo,kabla Nyanga,alikuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Mhe,Abdilah Jihad Hassan,kuwa Waziri wa Mifugo na Uvuvi,leo Ikulu Mjini Zanzibar,kabla Jihad alikuwa Waziri wa Habari,Utalii, Utamaduni na Michezo.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri aliowaapisha waliosimama,hafla hiyo imefanyika leo Ikulu Mjini Zanzibar,wengine Makamo wa kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif,(kushoto) na Makamo wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi,(kulia).
========= ======== =======
Na Fakih H. Mbarouk MAELEZO ZANZIBAR.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Muhammed Shein leo amewaapisha mawaziri Sita (6) wa Wizara mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Mshauri wa Rais Pemba huko IKULU Mjini hapa..
Walioapishwa ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Ali Juma Shamuhuna,Waziri wa Kilimo na Maliasili Mhe. Suleiman Othman Nyanga na Waziri wa Ardhi Makaazi Maji na Nishati. Mhe. Ramadhani Abdalla Shaaban
Wengine ni Waziri wa Uvuvi na Mifugo Mhe. Abdilahi Jihadi Hassan, Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Mhe. Said Ali Mbarouk na Mhe. Mansour Yusouf Himid ambaye ni Waziri asiyekuwa na Wizara Maalum. Halkadhalika amemuapisha Bwana Sheha Moh”d Sheha kuwa mshauri wa Rais Kisiwani Pemba.
Katika sherehe hizo za kuwaapisha Mawaziri hao zilihudhuriwa na Viongozi mbali mbali akiwemo Makamo wa Kwanza wa Rais maalim Seif Sharif Hamad , Makamo wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zaznibar Mhe. Omar Othman Makaungu , Spika wa Baraza la Wawakilishi Pandu Amei Kificho, Mawaziri na viongozi wengine .wa serikali.
Kuapishwa kwa mawaziri hao kunafuatia mabadiliko yaliyofanywa juzi na Raisa wa Zanzibar Dk Ali Muhammed Shein ambao Mawaziri hao walibadilishwa Wizara.
0 comments:
Post a Comment