Nafasi Ya Matangazo

January 14, 2025

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Januari 14, 2025 amefanya mazungumzo na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa  Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe aliofuatana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam. 

Katika mazungumzo yao, Waziri Mkuu amemweleza Mheshimiwa Fujii kuwa Tanzania imeendelea kuweka mazingira rafiki ya kufanya uwekezaji ambayo yanawawezesha wawekezaji kunufaika na shughuli zao.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa  Fujii Hisayuki (kulia kwake) na ujumbe aliofuatana nao kwenye ukumbi wa Mikutano wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, Januari 14, 2025. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akimkabidhi zawadi ya picha  Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan wa Japan Mheshimiwa Fujii Hisayuki baada ya mazungumzo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam, January 14, 2025. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika picha ya pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Japan, Mheshimiwa Fujii Hisayuki (kulia kwake) baada ya mazungumzo kwenye ukumbi wa Ofisi Ndogo ya Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar es salaam. Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Cosato Chumi na kulia ni Balozi wa Tanzania chini Japan, Baraka Luvanda. Kushoto ni Balozi wa Japan nchini, Yusushi  Misawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Posted by MROKI On Tuesday, January 14, 2025 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo