Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akimfariji mjane wa aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Coperation, marehemu, Danny Mwakiteleko, Winfrida, alipokwenda kuhani msiba nyumbani kwa marehemu, Tabata Chang'ombe, Dar es Salaam. Mwakiteleko alifariki dunia juzi katika Hospitali ya Muhimbili alikolazwa baada ya kupata ajali Jumatano usiku. Mwili wa Mwakiteleko unasafirishwa leo kwenda nyumbani kwao Ndala, Mwakaleli, Tukuyu, kwa mazishi. Mke wa Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa, Regina (kushoto) akiwafariji watoto wa alipokwenda kwenye msiba wa aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Coperation, marehemu, Danny Mwakiteleko,Vanesa na Caroline Mwakiteleko, alipokwenda yeye na mumewe kuhani msiba nyumbani kwa marehemu
Wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa msibani.
Baadhi ya waombolezaji wakiwa nyumbani kwa mareheu.
Kaka nikusalimie...Waziri Mkuu mstaafu, Edward Lowassa (kushoto) akisalimiana na Mhariri Mtendaji wa gazeti Mwanahalisi, Said Kubenea walipokutana jana kwenye msiba wa aliyekuwa Naibu Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya New Habari Coperation, marehemu, Danny Mwakiteleko, Tabata Chang'ombe, Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Habari Coperation. Hassan Bashe.




0 comments:
Post a Comment