Kama ilivyo kwa timu za Mpira zifanyapo usajili kuboresha timu ndivyo hata Makampuni mbalimbali yamekuwa yakifanya ili kuboresha huduma na kupata mafanikio zaidi. Hivi karibuni Kampuni ya Bia ya Serengeti ilifanya Usajili wa maana na uliostua wengi hasa wafanyao biashara moja. Usajili huu ni pale walipo msajili Kiungo Mchezeshaji, Mkurugenzi wa Masoko EPHRAIMU MAFURU. Mafuru alikuwa Mchezaji huru baada ya kukacha usajili wa Vodacom msimu uliopita. Mafuru aliwahi kufanya kazi katika TBL miaka ya nyuma.
Hii ni leo katika Uwanja wa Mkwakwani mjini Tanga, ambapo mafuru alionekana akiwa katiika jezi ya Serengeti Fiesta 2011.




0 comments:
Post a Comment