
Vodacom Miss Tanzania 2009, Miriam Jerry akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 9 kutoka kwa Ofisa Mkuu wa Mahusiano wa kampuni ya Vodacom Group (Vodacom Group Chief Officer of Corporate Affairs, Bob Collymore ikiwa ni moja ya zawadi kwa kutwaa ushindi huo wakati wa hafla ya kuwapongeza iliyofanyika kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam juzi. Zawadi za fedha za washindi wa shindano hilo zitaingizwa katika akaunti zao zilizofunguliwa katika benki ya Kenya Commercial Bank.

Mshindi wa pili wa Vodacom Miss Tanzania 2009, Beatrice Lukindo akitabasamu baada ya kupokea mfano wa hundi ya shs milioni 6.2.
Mshindi wa tatu wa Vodacom Miss Tanzania 2009, Julieth William akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 4.
Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki ya Kenya Commercial Bank, Christina Manyenye akitambulishwa katika hafla ya kuwapongeza washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2009.

Baadhi ya wadau wa urembo wakiselebuka na baadhi ya washindi na washiriki wa shindano la Vodacom Miss Tanzania 2009 katika hafla ya kuwapongeza kwenye Hoteli ya Giraffe, Dar es Salaam juzi.

Meneja wa Bia ya Redds Kabula Nshimo(kulia)akimkabidhi Vodacom Miss Tanzania 2009 Miriam Gerald zawadi ya mfano wa hundi ya shs milioni moja baada ya kuibuka mshindi wa shindano la Miss Redd's Photogenic 2009.
0 comments:
Post a Comment