Nafasi Ya Matangazo

September 22, 2009

Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein akitia saini kitabu cha maombolezo jana, kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Anita Ngowi aliyefariki juzi nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam leo.
Mke wa Makamu wa Rais, Mwanamwema Shein akitia saini kitabu cha kumbukumbu kufuatia kifo cha aliyekuwa Mkurugenzi wa Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais marehemu Anita Ngowi.
Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohamed Shein, akimfariji Walter Ngowi mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais, Anita Ngowi aliyefariki juzi nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam baada ya kuuguwa ugonjwa wa Saratani , mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa jana alasiri katika makaburi ya Kinondoni Dar es salaam.
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein, akimfariji Miriam Ngowi ambaye pia ni mtoto wa marehemu
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Ali Mohamed Shein akimfariji Clifford Ngowi mtoto wa
marehemu Anita Ngowi
Makamu wa Rais Dk. Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein wakitowa heshima za mwisho kwenye jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Muungano katika Ofisi ya Makamu wa Rais marehemu Anita Ngowi aliyefariki Dunia juzi nyumbani kwake Oysterbay Dar es salaam kutokana nakuuguwa ugonjwa wa Saratani, mwili wa marehemu unatarajiwa kuzikwa leo alaasiri katika makaburi ya kinondoni Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Tuesday, September 22, 2009 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo