Nafasi Ya Matangazo

May 07, 2024

 Idadi ya Watu wanaojua kusoma na Kuandika kuanzia umri wa miaka Mitano nchi imeongezeka maradufu kutoka asilimia 44 hadi asilimia 83 kwa sasa.

Mtakwimu Mkuu wa Serikali Dkt Albina Chuwa ametoa takwimu hizo katika semina ya Viongozi wa Wilaya ya Iramba kuhusu mafunzo ya usambazaji na Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 nchini.

Dkt Albina Chuwa amesisitiza matumizi sahihi ya takwimu hizo katika kupanga na kutelekeza shughuli za maendeleo katika jamii husika.

Amesema kuwa kwa Mkoa wa Singida idadi ya watu wanaojua kusoma na kuandika pia imepanda hadi kufikia asilimia 70 ambapo wilaya ya Iramba ni asilimia 68.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda amemhakikishia Mtakwimu Mkuu wa Serikali kuwa watatumia takwimu hizo vizuri katika kupanga na kuboresha huduma za kijamii katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo.



Posted by MROKI On Tuesday, May 07, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo