Nafasi Ya Matangazo

March 25, 2024

Mshindi wa kwanza wa Mashindano ya Kimataifa ya Quran Tukufu Afrika ya 24 kwa mwaka 2024 kutoka Nchini Avory Coast  Ibrahim Sow, ameibuka mshindi wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Alhikma Foundation Tanzania yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini  Dar es Salaam leo 24-3-2024.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi  akihutubia katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, wakati wa Mashindano ya Kimataifa  ya Quran Tukufu  Afrika ya 24, yaliyofanyika katika Uwanja huo leo 24-3-2024
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi mshindi wa Kwanza wa Mashindani ya Kimataifa ya Quran Tukufu Afrika ya 24 kutoka Nchini Avory Coast Ibrahim Sow (kulia kwa Rais) mashindano hayo yaliyofanyika  katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam leo 24-3-2024.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi zawadi Mshindi wa Pili wa Mashindano ya Kimataifa ya Quran Tukufu Afrika ya 24, kwa mwaka wa 2024 kutoka Nchini Uganda Haafith Abdulkariim Kabiito, mashindano hayo yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam leo 24-3-2024.(Picha na Ikulu)

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhajj Dk.Hussein Ali Mwinyi akikabidhiwa zawadi maalum ya Msahafu na Rais wa Taasisi Alhikma Foundation Tanzania Sheikh Said Abdulkadir, baada ya kumalizika kwa Mashandano ya 24 ya Kimataifa ya Quran Tukufu Afrika, yaliyofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam leo 24-3-2024.
Wageni waalikwa katika mashindano ya Kimataifa ya 24 ya Quran Tukufu Afrika yaliyoandaliwa na Taasisi ya Alhikman Foundation Tanzania,wakifuatilia mashindano hayo yaliyofanyika katika uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam leo 24-3-2024.(Picha na Ikulu)

Washiriki wa Mashindano ya Kimataifa ya 24 ya Quran Tukufu Afrika wakiwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, leo 24-3-2024, wakati wa mashindano hayo yaliyoandaliwa na Taasisi ya Alhikman Foundation Tanzania.

Posted by MROKI On Monday, March 25, 2024 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo