Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akikabidhiwa Cheti mara baada ya kutunukiwa Shahada ya Udaktari wa Falsafa wa Heshima ikiwa ni Shahada ya Udaktari wa Juu katika Humanitia na Sayansi Jamii na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika Mahafali ya Hamsini ana mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akizungumza na viongozi pamoja na Wahitimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wakati wa Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolph Mkenda, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa William Anangisye kwenye picha ya pamoja na viongozi wengine wakati wa Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika tarehe 30, Novemba, 2022.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa pamoja na Wahitimu mbalimbali wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya Hamsini na mbili (52) ya Duru ya Tano ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mlimani City tarehe 30, Novemba, 2022.
**********
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia
Suluhu Hassan, ametoa wito kwa Vyuo Vikuu kupitia mitaala yake ili ijikite katika kutoa elimu
ambayo inakidhi mahitaji ya jamii.
Rais Samia ametoa wito huo leo mara baada ya kutunukiwa
Shahada ya Heshima ya Udaktari (Doctor of Letters - Honoris Causa) ya Chuo
Kikuu cha Dar es Salaam katika Mahafali ya 52 Duru ya Tano ya Chuo hicho yaliyofanyika
katika Ukumbi wa Mlimani City.
Aidha, Rais Samia amesema mitaala hiyo itawezesha
kutoa elimu ambayo inalenga kutoa wahitimu wenye weledi, wanaoajirika na
wajasiriamali.
Rais Samia amesema pamoja na kuwa na uhuru wa
kitaaluma, vyuo vikuu vina wajibu wa kutoa mchango wake katika kuleta
maendeleo, kutoa elimu stahiki, kufanya tafiti na kutoa maoni ili kulikuza na
kuliimarisha taifa letu.
Rais Samia pia amesema elimu inayotolewa na taasisi za
elimu ya juu inapaswa kuwawezesha wahitimu kujiajiri, kuajiriwa, kuwa
wajasiriamali na kuwa tayari kuchangia maendeleo ya taifa letu.
Vile vile, Rais Samia
amevitaka vyuo vikuu kuwa
na mikakati na malengo yanayolenga kufikia juu zaidi katika mzani wa kimataifa.
Hali kadhalika, Rais Samia
amesema Serikali inafuatilia na kutoa mchango kwa kuweka Sera na mikakati
ambayo inajumuisha kuendelea kuongeza bajeti ya elimu.
0 comments:
Post a Comment