Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akisikiliza maelezo kuhusu idara ya uchambuzi wa sera kutoka kwa Mchumi Bi. Jesca Mugyabuso kutoka Wizara ya Fedha na Mipango pindi alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akisikiliza maelezo kuhusu Mfumo wa Kieletroniki wa Ulipaji wa Huduma za Serikali (GePG) kutoka kwa Afisa Tehama Mwandamizi wa Wizara ya Fedha na Mipango, idara ya Usimamizi wa Mifumo ya Kifedha Bw. Zuberi Msisi, alipotembelea Banda la Wizara hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akisikiliza maelezo kuhusu Taasisi ya UTT AMIS kutoka kwa Afisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Taasisi hiyo Bi. Martha Mashoku, pindi alipotembelea Banda la Taasisi hiyo katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akimsikiliza kwa umakini Mhadhiri wa Chuo cha Mipango ya Maendeleo Vijijini Bw. Christopher Mdoe, pindi alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Maendeleo ya Taifa Dkt. Nicolaus Shombe, akimsikiliza kwa umakini Mhitimu na Mjasiramali kutoka Chuo cha Uhasibu (TIA) Bw. Isaya Maligite, pindi alipotembelea Banda la Chuo hicho katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam.
***********
Wizara ya
Fedha na Mipango ni moja ya washiriki katika Maonesho ya 46 ya Kimataifa ya
Biashara ya Dar es Salaam maarufu kama Maonesho ya Sabasaba.
Katika maonesho
hayo Wizara, imeshiriki pamoja na baadhi
ya Taasisi zake zikiwemo Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB), Kampuni
ya Uwekezaji ya UTT- AMIS, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana(CMSA), Soko
la Bidhaa Tanzania (TMX), Tanzania Commercial Bank( TCB), Hazina Saccos, Mfuko
wa Self, Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini (GPSA), Mamlaka ya Kudhibiti
Ununuzi wa Umma (PPRA), Mamlaka ya Rufaa ya Zabuni za Umma (PPAA), Ofisi ya
Taifa ya Takwimu (NBS), Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA), Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa
Hesabu Tanzania (NBAA), Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Chuo cha Mipango ya
Maendeleo Vijijini (IRDP) na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA).
Wizara na
Taasisi zake inashiriki katika maonesho haya kwa lengo la kutoa elimu kwa umma.
Maonesho haya
ya 46 ya Kimataifa ya Biashara yalianza rasmi tarehe 28 Juni 2022, yanatarajiwa
kufungwa 13 Julai, 2022.
0 comments:
Post a Comment