Nafasi Ya Matangazo

September 28, 2021

Aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Mhe. William Tate Ole Nasha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Mhe. William Tate Ole Nasha aliyefariki Dunia tarehe 27, Septemba, 2021 Jijini Dodoma.

Mhe. Rais Samia amemuelezea Marehemu Ole Nasha kuwa alikuwa mchapakazi na hodari katika sekta aliyokuwa na mtumishi mwaminifu wa Serikali na pia  ametoa mchango mkubwa katika ujenzi wa Taifa.

Mhe. Rais Samia ametoa pole kwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Yustino Ndugai, Wabunge, familia ya Marehemu na Wananchi wa Ngorongoro.

Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.

Posted by MROKI On Tuesday, September 28, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo