Nafasi Ya Matangazo

July 30, 2021

 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wawili kama ifuatavyo-

1.    Amemteua Bwana Rogatus Hussein Mativila kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Bwana Mativila anachukua nafasi ya Marehemu Mhandisi Patrick Mfugale ambaye alifariki dunia tarehe 29 Juni, 2021.

Kabla ya uteuzi huo Bwana Mativila alikuwa Mkurugenzi wa Barabara, Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi).

2.    Amemteua Prof. Yunus Daud Mgaya kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).

Prof. Mgaya ni Mkurugenzi Mkuu, Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR).

 Uteuzi huo umeanza tarehe 28 Julai, 2021.


Posted by MROKI On Friday, July 30, 2021 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo