Nafasi Ya Matangazo

January 19, 2018

Mwandishi Wetu, TJNCDF

Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza Tanzania (TANCDA) limekuwa likitoa elimu kwa ajili ya kuelimisha jamii juu ya magonjwa sugu.

Lengo ni kuiwezesha jamii kuwa na elimu sahihi juu ya namna ya kuyaepuka au njia sahihi za kuyadhibititoa kwa wale ambao tayari wameathirika.

TANCDA inaamini kwamba jamii ikiwa na uelewa wa magonjwa sugu yasiyo ya kuambukiza ni namna sahihi ya kuiokoa jamii ya sasa na vizazi vijavyo.

Tafiti mbalimbali zinaonyesha kuwa kadri miaka inavyoongezeka kasi ya watu kupata magonjwa haya inaongezeka na inasababisha adha nyingi zikiwamo kupunguza nguvu kazi, kutumia raslimali nyingi za fedha na kusababisha vifo.

Magonjwa sugu ya mfumo wa hewa ni miongoni mwa magonjwa yasiyo ya kuambukiza ambayo TANCDA inayawekea kipa umbele katika kuielimisha jamii.
§1
TNCDA katika moja ya vipeperushi vyake vya kuielimisha jamii, inaeleza kuwa magonjwa sugu ya mfumo wa hewa na mapafu hutokana na kuziba kwa njia ya hewa na kusababisha mtu apumue kwa shida.

Inaeleza kwamba kwa kawaida mtu anapozaliwa kinga ya mwili inakuwa na mfumo wa kuzoea vitu kwenye mazingira yetu na kuishi navyo bila shida.

Sababu moja ya pumu ni hali ambapo uzoefu na vitu kadhaa haukutosha hivyo kusababisha njia ya hewa kuchukua tahadhari ambazo madhara yake ni kuziba kwa njia ya hewa. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI MAKALA HAYA

Vitu vinavyoweza kusababisha hali hiyo itokee ni kama vile vumbi, mende, chavua, magamba au manyoya ya wanyama.

Vitu vingine ni kama vile moshi wa sigara, hewa chafu, harufu kali, msongo wa mawazo, dawa na baadhi ya kemikali.

Maelezo ya kitaalamu yanaonesha pia mtoto ambaye ametunzwa katika mazingira ambayo ni ya usafi wa hali ya juu anaweza kupata matatizo ya mfumo wa hewa iwapo baadaye ataishi katika mazingira ya vumbi, au vichocheo vingine ambayo mwili unakuwa haujayazoea.

TANCDA inatahadharisha kuwa, licha ya pumu hewa chafu nayo inaweza kuathri njia ya hewa na kuzifanya zizibe na kumfanya mtu kupumua kwa shida.

Miongoni mwa hewa chafu ni ile yenye moshi wa sigara. Moshi huo una kemikali nyingi zinazoathiri njia ya hewa na hata mishipa ya damu.

Dalili ni kwamba zinarudia rudia na hizo ni pamoja na kubana pumzi, kukosa hewa, kupumua harakaharaka na kukohowa.

TANCDA inaifahamisha jamii kuwa inaweza kujikinga na pumu kwa kuchukua hatua zifuatazo: Usafi wa nyumba na mazingira ili kupunguza vumbi na epuka moshi wa sigara kwa kutovuta au kukaa karibu na wavutaji kwa maana sehemu ambayo moshi unakufikia.

Hatua nyingine zinaelezwa kuwa ni kuepuka moshi kwa kutoishi eneo lenye moshi wa takataka au kutumia majiko yanayosababisha hali hiyo na inashauriwa kutoishi nyumba moja na wanyama.

Iwapo una pumu jitahidi kukwepa vitu vinavyosababisha hali hiyo na hudhuria kliniki kikamilifu na fuata maelekezo ya daktari juu ya namna bora ya kuishi na ugonjwa.


Makala haya yameandaliwa na Chama cha Waandishi Wanaopambana na Magonjwa Yasiyo ya Kuambukiza (TJNCDF). Maoni, ushauri au maswali tuma tjncdf@gmail.com au S.L.P 13695, Dar es Salaam.
Posted by MROKI On Friday, January 19, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo