Nafasi Ya Matangazo

January 19, 2018

Naibu Waziri Madini, Doto Mashaka Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Wachimbaji wadogo wa dhahabu katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri, Doto Biteko kwenye mkutano wa hadhara wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi, Leo 8 Januari 2018.
Naibu Waziri Madini  Doto Biteko akikagua mgodi wa kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) kabla ya kuzungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.
Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko akikagua baadhi ya maeneo ya uzalishaji madini ya dhababu kwenye kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi. BOFYA HAPA KUSOMA ZAIDI. 

Naibu Waziri Madini, Doto Biteko akizungumza na wachimbaji wadogo kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela Wilaya ya Ruangwa wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi
******************
Na Mathias Canal, Lindi
NAIBU Waziri wa Madini, Doto Biteko amemtaka Kamishna msaidizi wa madini Kanda ya Kusini, Mayigi Makorobela kufungua ofisi ya Madini Wilayani Ruangwa ikiwemo kupeleka wataalamu ili kurahisisha huduma za kitaalamu kwa wachimbaji wadogo ikiwemo elimu ya usalama kazini haraka iwezekanavyo.

Biteko ametoa agizo hilo  Januari 18, 2018 wakati akizungumza na wachimbaji wadogo waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara katika kitongoji cha Namungo Kata ya Megembekenyela wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Lindi.

Alisema kuwa Wizara ya Madini imeamua kuanzisha ofisi hiyo kutokana na maagizo ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyoyatoa hivi karibuni wakati alipokuwa ziarani Mkoani humo ambapo alibaini kuwa wachimbaji wadogo wanapata kadhia kubwa kutokana na umbali wa ofisi kwani wanalazimika kutumia zaidi ya kilomita 45 kuzifikia ofisi za madini zilizopo Wilayani Nachingwea.

Alisema Serikali kwa ujumla inawapenda wachimbaji wadogo na hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu Rais John Magufuli alibainisha kukusudia kuwanufanisha watanzania kupitia rasilimali zao ikiwemo madini.

"Rais Magufuli anataka wananchi wote wanaoishi karibu na mgodi kunufaika na rasilimali zao, nyote mtakuwa mashahidi, tangu nchi iliporuhusu uchimbaji wa madini hakuna manufaa ya moja kwa moja kwa watanzania badala yake madini yamekuwa yakinufaisha mataifa mengine ambayo baadaye tunayapigia magoti kuyaomba msaada" Alisema Naibu Waziri Biteko.

Biteko alisema kuwa lengo la kuanzisha ofisi ya madini katika Wilaya hiyo ya Ruangwa ni kuwarahisishia wachimbaji kuwa na jukumu moja la kuchimba na kuuza rasilimali wanazozipata kwani watakuwa sehemu ya kuchagiza maendeleo sambamba na kuinufaisha serikali kutokana na ulipaji kodi.

Aliwasihi wachimbaji hao kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Dkt John Magufuli kwani tangu ameingia madarakani katika kipindi kifupi ameimarisha nidhamu mpya kwa kila mtanzania na usimamizi madhubuti wa rasilimali za Taifa.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri wa Madini, Doto Biteko ameipongeza kampuni ya uchimbaji dhahabu na Green Garnet ya Gemini Exploration & Mining Services (GEMS) ambayo ni kampuni ya wazawa kwa kufanya kazi kwa kufuata vyema sheria na taratibu za uchimbaji.

Alisema kuwa kampuni zingine zinapaswa kujifunza kwa kampuni hiyo ya GEMS kutokana kulipa kodi mbalimbali kwa uwazi na ushiriki wa shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kusaidia sekta ya afya, Maji, sekta ya elimu sambamba na michezo.

Posted by MROKI On Friday, January 19, 2018 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo