Nafasi Ya Matangazo

November 07, 2017

 Dar Teknohama Business incubator – DTBi trainee Edmund Sepeku speaks to Kijitonyama Kisiwani primary School pupils during an event to introduce ICT knowledge to teachers and pupils of the school, a programme which is a partnership between Airtel Tanzania and DTBi
 Airtel Tanzania Project Manager Jane Matinde shows Kijitonyama Kisiwani primary School pupils how a lego Robotics works during an event to introduce ICT knowledge to teachers and pupils of the school, a programme which is a partnership between Airtel Tanzania and DTBi.
 Dar Teknohama Business incubator – DTBi trainee Edmund Sepeku speaks to Kijitonyama Kisiwani primary School pupils during an event to introduce ICT knowledge to teachers and pupils of the school, a programme which is a partnership between Airtel Tanzania and DTBi
 A cross-section of Kijitonyama Kisiwani primary School pupils follow the proceedings of introduction ICT knowledge to teachers and pupils of the school, a programme which is a partnership between Airtel Tanzania and DTBi.
ICT Lab Airtel Fursa Manager Agape Jengela speaks to to Kijitonyama Kisiwani primary School pupils during an event to introduce ICT knowledge to teachers and pupils of the school, a programme which is a partnership between Airtel Tanzania and DTBi
**************
SHULE za msingi za Manispaa ya Kinondoni zimeshauriwa kutumia fursa ya maabara ya kompyuta iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama iliyopo kwenye manispaa hiyo ili kuweza kujifunza na kupata ujuzi wa Tehama kwa waalimu na wanafunzi pia.

Wito huo umetolewa na Meneja Miradi Airtel Tanzania Jane Matinde wakati akiongea na waalimu na wanafunzi wa shule ya msingi ya Kijitonyama Kisiwani baada ya kuitembelea na kutambulisha maabara hiyo. Maabara hiyo ni ushirikiano kati ya kampuni ya Airtel na Atamizi ya Teknohama ya Dar es Salaam (DTBi) kuhakiksha kuwa Jamii inakuwa na uelewa wa Tehema kwa mafanikio yao na taifa kwa ujumla.

Tunayo Idadi kubwa ya waalimu na wanafunzi ambao Tayari washaanza kupata mafunzo hayo lakini wengi wao wametokea kwenye shule ya Kijitonyama ambapo hii maabara ipi. Naomba kutoa wito wangu na nyinyi mtumia hii fursa na mpate mafunzo ya Tahema na ikizingatiwa shule hizi ni majirani.

Ni furaha kwa wanafunzi hawa kupata mafunzo ya Tehama kwa umri mdogo kwani inawaraihishia maisha yao ya masomo ya baadae. Pia, kuna wanafunzi wengine wanakuwa na uelewa mkubwa kwenye mafunzo ya matendo kuliko nadharia, hii ndio sehemu pekee kwa wanafunzi wa shule ya msingi kupata mafunzo hayo, aliongeza Matinde.

Matinde aliongeza kuwa bado mafunzo yataendelea hata baada kuwa shule zimefungwa kwa ajili ya likizo ya krismas na mwaka mpya na hivyo wito kwa vijana wa sekondari , wale waliomaliza darasa la saba , wafanyabiashara kutumia vyema maabara hii yenye lengo la kuwezesha jamii  hususani vijana kuongeza ujuzi na ueledi kwenye maswala ya technologia na Tehama kwa ujumla.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu msaidizi wa shule ya Kijitonyama Kisiwani Sikudhani Semka alitoa shukrani kwa kampuni ya Airtel kuweza kuwatembelea na kuitambulisha maabara hiyo shuleni kwake. ‘Nachukua fursa hii kuwashukuru wenzetu wa Airtel. 

Hapa shuleni kwetu tunao kompyuta tano lakini hakuna hata moja ambayo inatumika sababu ikiwa hakuna mwalimu mwenye ujuzi wa kuitumia. Tutamia fursa na kujifunza mambo ya Tehema ili na sisi tuende na wakati, alisema Semka.

Kwa upande wake Meneja wa maabara ya Airtel Fursa, Agape Jengela alisema “Tayari tumejipanga kutoa mafunzo kwa yeyote ambaye atayejiunga nasi. Tuhahakisha kuwa kila anayekuwa anapata mafunzo ya hali ya juu na kuelewa kabisa ili nao waweze kutoa mafunzo na elimu kwa wanafunzi wenzao

Jengela alisema mafunzo yanayotolewa ni pamoja na lego Robotics, program za uhuishaji kwa watoto(ziitwazo scratch) na ubunifu na uchapishaji wa“3D objects”  msingi wa kompyuta, uelewa wa kompyuta, kutengeneza program mbali mbali

Bado tunapokea maombi,   Tunato wito kwa wazazi na walezi kuwaandikisha vijana wao kwa kupitia  www.teknohama.or.tz na  www.airtelfursa.com  au kwa kutembelea maabara  iliyopo katika shule ya msingi Kijitonyama
Posted by MROKI On Tuesday, November 07, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo