Nafasi Ya Matangazo

March 10, 2017




 MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa
Na Rhoda Ezekiel Kigoma,
MKUU wa Wilaya ya Kakonko, Kanali Hosea Ndagala ameahidi kuwachukulia hatua wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa endapo watashindwa kukamilisha miradi hiyo  kwa wakati  ilikuondoa upungufu wa vyumba vya madarasa.

Maagizo hayo aliyatoa jana wakati akikagua ujenzi wa madarasa manne na ofisi mbili katika Shule ya Msingi Kakonko Wilayani humo ambapo alibaini kuwepo kwa tatizo la ucheleweshwaji wa vifaa vya ujenzi kwa mafundi hali inayo pelekea kusua sua kwa ujenzi huo.

Mkuu huyo alisema mradi huo ulitakiwa kuwa umekabidhiwa lakini mpaka sasa mradi huo bado haujakamilika kutokana na uzembe wa baadhi ya wasimamizi Wa mradi huo kushindwa kuwasimamia mafundi ipasavyo waweze kukamilisha ujenzi huo, na ifikapo mwezi wa tatu Mwishoni  ujenzi huo uwe umekamilika na wanafunzi wapate madarasa yao waendelee kuyatumia.

" niwatake Wahandisi wa halmashauri kwa kushirikiana na Watendaji wa kijiji kuwasimamia mafundi kwa karibu ilikuhakikisha mradi huu unakamilika kwa wakati endapo mtashindwa kusimamia ipasavyo tutawajibishana, Wananchi wamejitahidi kuchangia na Serikali imetoa fedha kwa wakati ni lazima muhakikishe mnakamilisha suala hili ilikuwatia moyo wananchi kuendelea kuchangia jitihada za Serikali",alisema Kanali Ndagala.

Hata hivyo Ndagala alisema katika Wilaya hiyo kunaupungufu wa madarasa ambapo mpaka sasa juhudi za kumaliza changamoto hiyo inaendelea  kwa kuhakikisha Wananchi wanachangia kwa kushirikiana kujenga na kufyatua tofari na serikali inasaidi a kiasi kidogo cha fedha pamoja na kuezeka bati katika majengo hayo.

Kwa upande wake Mkuu wa Shule ya Msingi Kakonko, Novatus  kalobagwa alisema Shule hiyo inazaidi ya Wanafunzi 1000 na ina madarasa tisa ambapo matano yamekamilika na manne yanaendelea kujengwa , hali hiyo inapelekea kila darasa kuwa na Wanafunzi 100-105 hali inayo pelekea mwalimu kuwa na wakati mgumu katika ufundishaji.

Alisema kutokana na Changamoto hiyo bado Wanafunzi katika shule hiyo wanaendelea kufauru, ambapo mwaka jana Wanafunzi wote wa darasa la saba Walifauru kwa asilimia miamoja na watano walipelekwa katika shule za vipaji maalumu kutokana na ufauru wao kuwa mzuri.

Aidha aliiomba serikali kihakikisha inamaliza kero hiyo kutokana na Maelekezo ya elimu ni kwamba ilikuhakikisha Mwanafunzi anaelewa ni lazima darasa moja liwe na Wanafunzi 45 kila chumba ambapo itamsaidia mwalimu kujua maendeleo ya mwanafunzi mmoja mmoja na kuongeza ufauru kwa kiasi kikubwa.
Posted by MROKI On Friday, March 10, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo