Nafasi Ya Matangazo

March 09, 2017

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha, Lucia Mwiru akizungumza  jijini A rusha katika Kata ya Sekei.   wakati alipokuwa akizungumza na wanachama, mabalozi wa nyumba kumi, makatibu Kata,wazee maarufu  

Na Mwandishi wetu Arusha
Wanachama wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Arusha wametakiwa kuwaheshimu mabalozi wa nyumba kumi wanaotokana na chama hicho ili kuleta maendeleo ya kasi na yenye tija kwa wananchi hali ambayo itaongeza idadi ya wanachama wapya

Pia  wanachama hao wamesisitizwa kuacha majungu badala yake kuhakikisha wanaimarisha chama kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali sanjari na kufungua matawi na kugawa kadi mpya kwa wakati.

Hayo yalisemwa na  Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Arusha, Lucia Mwiru jijini A rusha katika Kata ya Sekei.   wakati alipokuwa akizungumza na wanachama, mabalozi wa nyumba kumi, makatibu Kata,wazee maarufu 

Alisema yeye ni mgeni katika wilaya hiyo na ndio maana anapita kila Kata kwaajili ya kuongea na wanachama wa CCM ikiwemo kuhakikisha kila jambo wanalolifanya ni lazima mabalozi wa nyumba kumi waheshimiwe ikiwemo kushirikishwa katika miradi mbalimbali ya chama.

Alikemea vikali  tabia ya baadhi ya wanachama kuwapuuza mabalozi  na kuwaona wanamaana kwenye chaguzi mbalimbali na mara ya chaguzi kuisha husaulika kabisa
.
Aidha alisema kuwa mabalozi ni watu muhimu sana katika chama hivyo wanahaki ya kuhusishwa katika miradi mbalimbali ya chama ili na wao wanufaike na keki iliyopo badala ya watu wachache kukumbatia keki hiyo

Pia alisema baadhi ya viongozi wa ccm wanafanya miradi ya chama kama shamba la bibi huku wanachama pamoja na viongozi wengine hawajui nini kinaendelea na hata wakihoji wanaambiwa kuwa ni wasaliti kwa kutengezewa maneno yasiyofaa.

Naye Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Mjini, Jasper Kishumbua alitoa rai kwa wanachama wa chama hicho Mkoa wa Arusha na kata mbalimbali kuongeza idadi ya wanachama pamoja na kufungua matawi ili kuongeza ari katika chama
 
Kwa upande wa wanachama waliokuwepo katika mkutano huo , Nehemia Mollel na Mariam Hussein walitoa rai kwa wanachama kujua wanachama wote wanaoishi kwenye kila Kata ili panapotokea masuala ya uchaguzi iwe rahisi kuwajua kwani baadhi ya wanachama wengine wanatoka Kata fulani kuja kupiga kura kwingine na kupelekea chama kushindwa.
Posted by MROKI On Thursday, March 09, 2017 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo