Nafasi Ya Matangazo

September 17, 2016

ZAIDI ya Shilingi Milioni 502.6 zimekusanywa hii leo jijini Dar es salaam katika matembezi maalum ya kuchagia waathirika wa tetemeko la ardhi mkoani Kagera. Matembezi hayo kilometa 5 yaliongozwa na Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi (wapili kushoto).

Wengine kutoka kushto ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Augustine Mahiga, Mbunge wa Muleba, Profesa Anna Tibaijuka, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk Susan Kolimba.
 Rais Mstaafu awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi akianzisha matembezi hayo.
 Washiriki wakijiselfisha kabla ya kuanza matembezi hayo.
 Wafanyakazi wa Kampuni ya Magazeti ya serikali TSN, wachapaji wa magazeti ya Daily News, Habarileo na Spotileo wakipozi kwa picha.
 Washiriki wakijiandikisha tayari kwa kushiriki maandamano hayo.
 Iran ni miongoni mwa nchi zilizounga mkono matembezi hayo.
  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadj Mussa Salum akitafakari kabla ya kuanza matembezi hayo.
 Balozi Liberata Mulala (kushoto) akizungumza na Profesa Anna Tibaijuka
 Mkuu wa Kitengo cha Mawasilino na Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Mindi Kasiga akipiga picha.
Father Kidevu nae ni miingoni mwa walioshiriki matembezi hayo, hapa akiwa na Prof Anna Tibaijuka na Balozi Liberata Mulamula wakipasha.
 Kupasha moto viungo. BOFYA HAPA KUONA MATUKIO ZAIDI.
 wadau wa tazara
 Kupasha moto viungo
 Balozi Dk Mahiga akizungumza
Rais Mstaafu Mwinyi akianzisha matembezi hayo
 Bendi ya Polisi ikiongoza matembezi hayo...

 PPF ni miongoni mwa Mashirika yaliyoshiriki kikamilifu
 Washiriki wa matembezi hayo wakitembea
 Mhariri Mtendaji wa Magazeti ya serikali Dk Jim Yonaz


 Wafanyakazi wa Magazeti ya Serikali TSN nao walishiriki kikamilifu katika matembezi hayo.
 Wadau Christina Manongi 'Sinta' na Dorice Molel walikua ni miongoni mwa watembeaji.
Balozi William Kallaghe ni miongoni mwa washiriki
 Huyu mwendo wa Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ulimshinda akapita njia ya mkato..
 Kituo cha Maji kilikuwepo.
 Benki ya Akiba nao walishiriki katika matembezi hayo
 Baada ya kumaliza matembezi walinyoosha viungo kidogo kujiweka sawa.
Mzee Hamisi Chifupa baba mzazi wa aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum, Marehemu Amina Chifupa akiwa na Mjukuu wake Rahman Mpakanjia baada ya kushiriki matembezi hayo na Rahman kuchangia elfu 50,000.
 Washiriki wa matembezi wakimsikiliza Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi aliyekuwa akihitimisha matembezi hayo.
Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi akifunga matembezi hayo. 
Posted by MROKI On Saturday, September 17, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo