Nafasi Ya Matangazo

August 20, 2016

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Simba, Laudit Mavugo leo alifungua pazia la magoli kwa timu ya Simba baada ya kuifungia goli la kwanza kati ya magoli matatu yaliyoipa ushindi wekundu hao wa Msimbazi.

Goli hilo la Simba kwa mpachika mabao huyo lilidumu hadi kunako dakika ya 38 pale Omar Mponda alipoisawazishia timu yake ya Ndanda FC bao lililodumu hadi kipindi cha kwnza kinaisha kwa 1-1.

Kipindi cha pilu kilianza kwa kasi kwa timu zote kushambuliana kwa.nguvu lakini Simba ndio walikua vinara kwa kupeka mashambulizi.memgi zaidi langoni mwa Ndanda kutoka Mtwara.

Ni dakika ya 73 ndipo Simba iliwadhihirishia mashabiki wake kua imetumwa Point uwanjani hapo baada ya mshbuliaji wake wa Kimataifa   Fedrick Blagnon, alipo wanyanyua vitini mashabiki wake kwa bao la pili. 

Alikua ni Shiza Kichuya aliyeithibitishia Sinb ushindi wa point 3 na goli 3 leo kufuatia shuti kali alilolipiga katika dakika ya 80 baada ya mlinda mlango wa Ndanda FC kuushindwa mpira wa kona alioupangua na kumkuta Kichuya aliyeukimiani bila ajizi. Hadi kipenga cha mwisho Simba 3 Ndanda 1.

Mbali na Simba na Ndanda FC matokeo ya michezo mingine leo hii ni kama ifuatavyo:- Ruvu Shooting  imeondoka na point tatu na goli 1 kwa Mtibwa iliyoambulia patupu, Prison 1 Maji Maji 0, Azam 1 Afican Lyon 1, Stand Unt 0 Mbao FC 0.

Kikosi kinachoanza leo Simba vp Ndanda FC:
1.Vincent Paul Angban 
2. Malika Ndeule
3. Mohamed Hussein 
4. Method Mwanjali 
5. Juuko Murshid 
6. Jonas Mkude 
7. Shiza Kichuya
8. Mohamed Ibrahim 
9. Laudit Mavugo 
10. Ibrahim Ajib Migomba
11.Jamal Mnyate 

Subs :

1. Manyika Peter 
2. Abdi Banda 
3. Hamad Juma 
4. Mousa Ndusha 
5. Mwinyi Kazimoto
6. Fedrick Blagnon
Posted by MROKI On Saturday, August 20, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo