Nafasi Ya Matangazo

February 04, 2016



Mabondia Mada Maugo kushoto na Abdallah Pazi wakitunishiana misuli baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa taifa Dar es salaam katikati ni mratibu wa mpambano uko kochwa wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' 
Bondia Abdallah Pazi kushoto akipokea sehemu ya fedha yake kwa ajili ya maandalizi ya mpambano wake na Mada Maugo utakaofanyika uwanja wa ndani wa taifa anaetoa fedha hizo ni mratibu wa mpambano uho Rajabu Mhamila 'Super D' 
Bondia Mada Maugo kushoto akipokea sehemu ya malipo ya awali kutoka kwa mratibu  Rajabu Mhamila 'Super D' wa mpambano wake na Abdallaha Pazi. utakaofanyika siku ya sikukuu ya Pasaka .

************
Na Mwandishi Wetu
Mabondia Mada Maugo na Abdalla Pazi 'Dulla Mbabe' wamesaini mkataba wa kuzipiga siku ya sikukuu ya pasaka katika uwanja wa ndani wa   taifa mpambano wa raundi nane KG 76.

akizungumza wakati wa kutiliana saini mikataba hiyo kocha wa mchezo wa masumbwi nchini ambaye ni mratibu wa mpambano uho

amesema kuwa amewasainisha mabondia hawo ambao wanatamba katika tasnia ya masumbwi nchini

ili wapenzi wa mchezo wa masubwi waburudike siku hiyo ya sikukuu ya pasaka

mbali na mpambano uho siku hiyo bondia chipkizi anaekuja kwa kasi zaidi katika mchezo wa masumbwi Vicent Mbilinyi anaetokea katika Super D  Boxing Promotion atakae pambana na Mwinyi Mzengela mpambano wa KG 63 raundi nane mpambano mwingine utawakutanisha bondia Cosmas Cheka na Mohamed Matumla na Pius Kazaula atakumbana na Seba Temba
 

siku hiyo kutakuwa na uzwaji wa DVD za ngumi  mabingwa wa Dunia akiwemo mpya za masumbwi kati ya bondia Amir Khan vs Nichlaus Maidana na Floyd mayweather vs Nichlaus Maidana one and two Manny Paquaio, Floyd Maywether, Roy Jones,Miguel Cotto,Linox Lewis, David Haye,Mohamed Ali.

“Ninatarajia kuwepo kwa ajili ya kuwauzia DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika Mpambano  ili kuweza kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi”, alisema Super D .
Posted by MROKI On Thursday, February 04, 2016 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo