Nafasi Ya Matangazo

November 29, 2015

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa kijamii wa PSPF Adam Mayingu (wapili kushoto) na Afisa Mahusiano wa mfuko huo Abdul Njaidi  wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5, Sarah Keiya (wapili kulia) na Meneja Biashara wa kituo hicho, Angela Maina.
*************
KAMPUNI ya Tan Communication Media inayomiliki kituo cha Radio 5  pamoja na mfuko wa kijamii wa PSPF imewafikia wadau wa mfuko huo kwa kuwapa elimu kupitia kipindi cha “Good-Morning Tanzania
 
Mkurugenzi mkuu wa mfuko huo Bw.Adam Mayingu akiongozana na Afisa mahusiano wa mfuko huo Bw.Abdul Njaidi walipokelewa na meneja Masoko na Mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah Keiya pamoja na Meneja Biashara wa kituo hicho Bi.Angela Maina
 
Akizungumza katika kipindi hicho kinachorushwa na kituo hicho Bw.Adam alisema kuwa ni wajibu wao kutoa elimu kwa jamii ili iweze kupata fursa ya kufahamu vema mfuko huo pamoja na kufaidika na huduma za afya za PSPF kupitia NHIF
 
Kwa upande wake Meneja masoko na mahusiano wa Radio 5 Bi.Sarah alisema uwepo wa mifuko ya kijamii inawezesha wananchi kupanga maisha yao ya sasa na baadae  na ndio maana Radio 5 imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mipango ya mifuko hii inawafikia walengwa
 
Bi,Sarah alisema kuwa Mkurugenzi wao Bw.Robert Francis amekuwa akiwezesha idara yao ya masoko na biashara kwa kutoa bei nafuu ya matangazo kwa mifuko hii ya kijamii ili kuwezesha kuwafikia wananchi kwa wingi na urahisi
Posted by MROKI On Sunday, November 29, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo