Nafasi Ya Matangazo

July 06, 2015



MWANDISHI wa habari ni mtu muhimu sana katika jamii, na wakati mwingine amekuwa akitambulika kama Mhimili wa nne usio rasmi wa serilali, ukiacha Bunge, Mahakama na Serikali.

Waandishi wapo mstari wa mbele sana kuhamasisha jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo, kupaza sauti juu ya kero mbalimbali zilizopo katika jamii hizo na hata watatuzi wa hizo kero ama serikali au makundi mengine katika jamii hizo kuona na kutafuta ufumbuzi wake.

Mwandishi wa habari ni mtu ambaye huitumia kalamu yake ama kujenga kitu au mtu na mtu huyo ama kitu hicho kuonekana ni bora zaidi kuliko vyote lakini pia kalamu hiyo hiyo Mwandishi anaweza kuitumia kuboa kabisa kile alichokijenga kwa sifa nyingi na jamii kuona huyu ndio mtu.

Hebu ona sasa hivi mwandishi wa habari hasa yule anayeaminika katika chumba fulani cha habari alivyo ‘lulu’ katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Rais, Wabunge na madiwani.

Kila mtu mwenye nia ya kutaka kugombea kuwania moja ya nafasi za uongozi anahaha kupata mwandishi ambaye kama si kuamuandika vizuri gazetini au kumtangaza vizuri na hao wapiga kura wake watarajiwa wakamsoma ili wamchague.

Ndio! Na waandishi wa wazuri wapo wengi sasa wadau hapa wanazidiana kete tu na mtu kutoka huku kwenda huku. Wapo wanaofanya kazi hiyo ya kuwapamba na kuwafagilia watu ilimradi tu aione kesho yake bila kujadi maadili au laa  lakini wapo wanaoifanya kazi hiyo kwa kuzingatia maadili.

Mwandishi wa habari amekuwa mbele sana katika kufanya mambo ya watu, lakini akijisahau yeye mwenye matatizo lukuki yanayo mkabili. Hebu angalia wafanyakazi wa kampuni fulani wagome kuhusiana na maslahi duni wanayopata au manyanyaso kwa mwajiri wao uone kesho watakavyo andika magazetini na kutangaza, lakini wamesahau kuwa wao ndio watu wa mwisho katika maslahi na hata hayo madogo wanayotakiwa kuyapata hawayapati kwa wakati.

Hivi sisi waandishi tumelogwa! Na kama ndio basi aliyetuloga hiyo tunguli kaitupa baharini na na mganga mwenye kujua tiba yake kafa. Haiwezekani tumeshindwa kujikingia kifua, ni waoga au nini kinatusibu hata kushindwa kupigania maslahi yetu? Jamani haya maslahi tunashindwa hata kusaidiana nako tunashindwa?SOMA ZAIDI HAPA
Posted by MROKI On Monday, July 06, 2015 1 comment

1 comment:

  1. Ni ukweli usiopingika, inatakiwa kuamka, kusimama pamoja na kuwa na sauti moja

    ReplyDelete

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo