Nafasi Ya Matangazo

July 06, 2015

TIMU ya Coast Union yenye maskani yake mjini Tanga, leo imefanya uchaguzi wake mkuu na kumchagua Dk Ahmed Ally Twaha kuiongoza Clabu hiyo.

Dk Twaha alipata kura 192 na kumshinda mpinzani wake Steven Mnguto aliyepata kura 11. huku nafasi ya makamu mwenyekiti ikienda kwa Salim Amir aliyepata kura 193 za ndio huku kura 9 zikimkataa.

Nafasi ya Wajumbe wa Kamati ya utendaji waliopita na kura zao kwenye mabano ni Hassan Omary Bwana (190), Hassan Ramadhan Muhsin (190), Abdallah ZubeiryAlly (188), Hussein Ally Mwinyi Hamis (185), Aggrey Ally Mbapu (179), Mohamed Rajabu (179) na Omary Hassan Mwambashi (144).
Posted by MROKI On Monday, July 06, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo