Nafasi Ya Matangazo

June 27, 2015


 Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson Kasenyenda akitoa wito kwa watanzania wote wenye mapenzi mema kujitokeza kwa wingi kushiriki katika harambee hiyo itakayofanyika katika viwanja vya Leaders club,siku ya Jumamosi Julai 4,2015 wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene.Kulia ni wajumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe na Angela Msangi.


 Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bw. Assah Mwambene akiwahamasisha waandishi wa habari kuimarisha mshikamano katika Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaosumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa.Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Grace Nakson


 Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Habari (MAELEZO) Bi. Zamaradi Kawawa ambaye ni mjumbe wa kamati ya kuratibu Harambee ya kuwachangia wanahabari wanasumbuliwa na magonjwa sugu ikiwemo kansa  akiwahamasisha wanahabari wote nchini kuungana katika harambee hiyo kwa kuihamasisha jamaii kushiriki katika tukio hilo muhimu. Kushoto  ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo  ugonjwa sugu wa saratani Bw. Benjamin Thompson.


 Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa kuhamasisha kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo  ugonjwa sugu wa saratani


. Mjumbe wa Kamati ya Kamati ya Maandalizi ya kuratibu Harambee ya kuwachangia waandishi wa habari wanaougua maradhi mbalimbali ikiwemo  ugonjwa sugu wa saratani Bi. Angela Msangi akiwahamasisha wanahabari kujitokeza kwa wingi katika harambee hiyo na pia kutumia taaluma yao kuihamasisha jamii kujitolea katika kufanikisha lengo la harambee hiyo. Kushoto ni Mjumbe wa Kamati hiyo Bi. Mwanamkasi Jumbe.
Posted by MROKI On Saturday, June 27, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo