Nafasi Ya Matangazo

June 27, 2015

 
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia (kushoto) na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo (kulia) kwa pamoja wakionyesha DVD za Filamu hiyo.
 
***********
Filamu ya Kiswahili ijulikanayo kama  Hamu ya Mafanikio ilizinduliwa rasmi  jana na Benki ya DCB katika Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam.
 
Filamu hiyo imeandaliwa na DCB Commercial Benki kwa kushirikiana na Kampuni ya ConsNet,yenye lengo la kuelimisha na kuhamasisha  wateja, wadau na umma kwa ujumla juu ya umuhimu na faida za kufanya shughuli za kibenki na DCB ambazo zinabadili maisha ya wateja kwa kiasi kikubwa.
 
Akizungumza katika uzinduzi huo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo amesema moja ya changamoto zilizopo katika sekta ya benki ni jamii kukosa elimu ya kutosha juu ya huduma za Kibenki,hivyo mbali na kujitangaza, DCB imeamua kutoa elimu ya kibenki  kupitia Filamu hiyo.
 
Kwa upande wake,Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia amewashukuru waandaaji wa Filamu hiyo,ikiwa  Bodi ya Filamu nchini pamoja na wasanii wote walioshiriki kuigiza filamu hiyo  kwa kazi nzuri waliyoifanya.
 
Pia ametoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya  kazi  yao kimakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
 
Washiriki katika Filamu hiyo ni pamoja na Tito Zimbwe,Rose Ndauka,Jackline Pentezel,Abdul Mhema,Hidaya Njaidi, Gojak na Wasanii wengine wengi. Baada ya kuzinduliwa Filamu hiyo itaonyeshwa katika maeneo mbalimbali ikiwemo City Centre,Magomeni,Arnautoglu,Mnazi Mmoja,Tabata,Ukonga,Chanika,Mabibo na Kariakoo kwa nyakati tofauti kuanzia Julai mwaka huu.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa DCB Commercial Bank, Samwel Dyamo akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Filamu ya Hamu ya Mafanikio 'Desire to Succeed' iliyozindulia katika ukumbi wa  Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa DCB, Balozi Paul Rupia akizungumza katika hafla  ya uzinduzi wa Filamu hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam jana ambapo alitoa wito kwa wasambazaji wa Filamu hiyo kuifanya  kazi  yao kwaumakini ili kutimiza malengo na madhumuni ya kuandaa Filamu hiyo.
Baadhi ya  washiriki na wadau waliohudhuria uzinduzi wa Filamu hiyo katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam,Juni 25,2015. Source: Michuzi Media
Posted by MROKI On Saturday, June 27, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo