Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2015



Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Abdulrahman Kinana (fulana ya njano) akipokelewa na Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa katika kata ya Makuyuni, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha leo tayari kwa kuanza ziara ya siku tisa ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na uhai wachama.
 *************
KATIBU Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana amemsifu Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Lowassa kwa kutekeleza kwa ukamilifu  ilani ya chama hicho Wilayani Monduli na kwamba anastaafu ubunge wake kwa heshima kubwa.


“Napenda kumpongeza Mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu yangu ,Edward Lowassa kwa kazi kubwa ya Maendeleo aliyofanya katika jimbio hili, maendeleo yote hapa hayakosi mkono wa Lowassa”, Alisema Kinana.

Kinana pamoja ameaza ziara ya kikazi mkoani Arusha baada ya kumaliza ziara ya mkoa wa Dodoma jana na aktika msafara huo anaambatana na Katibu Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Nnauye.

Msafara huo ulipokelewa katika Kata ya Makuyuni ambapo utakua mkoani Arusha kwa siku tisa. 


“ Ndugu lowassa ameamua kustaafu Ubunge na anaondoka kwa heshia kubwa, tunaklushukuru sana Lowassa kwa kazi hiyo kubwa ya kukisimamia chama kwa utekelezaji wa ilani yake. 
Posted by MROKI On Friday, March 13, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo