Nafasi Ya Matangazo

March 13, 2015

AJALI mbili zimetokea hii leo katika mikoa tofauti na kuyahusisha mabasi ya Arusha Express na ile ya Simuyu Express na kusababisha vifo.

Basi la Arusha Express lilipata ajali katika Eneo la Kisongo Airport nje kidogo ya mji wa Arusha baada ya kugongana na lori na kwa mujibu wa taarifa kutoka eneo la tukio zinaarifu kuwa Mtu mmoja aliyekuwa kwenye lori amefariki dunia huku watu wengine wanne wamejeruhiwa. Basi hilo lilikuwa likitokea Arusha kwenda Mbeya.

Huko Mkoani Simiyu napo Basi la Simuyu lifanyalo safari zake kati ya Dar es Salaam na Simiyu limegonga mkokoteni unaovutwa na Ngo'ombe na kusababisha kifo cha mtu mmoja na Ng'ombe wawili kufa papo hapo.
Mwonekano wa Basi la Arusha Express baada ya kugongana na Lori la mizigo.
Basi la Simiyu Express lililopata ajali hii leo.
Ng'ombe wakiwa wamekufa baada ya kugongana na basi la Simiyu hii leo. 
Posted by MROKI On Friday, March 13, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo