Nafasi Ya Matangazo

March 20, 2015

Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kushoto) msaada wa tani saba na nusu za saruji kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua yam awe yaliyotokea kijiji cha Mwakata Wilaya ya Kahama. Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi (kulia) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kushoto) msaada wa tani saba na nusu za saruji kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokana na mvua yam awe yaliyotokea kijiji cha Mwakata Wilaya ya Kahama.
Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kulia) akitoa shukrani kwa Benki ya Posta mara baada ya kupokea msaada wa tani saba na nusu za mifuko ya saruji zilizotolewa na benki hiyo. Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Benson Mpesya (kulia) akitoa shukrani kwa Benki ya Posta mara baada ya kupokea msaada wa tani saba na nusu za mifuko ya saruji zilizotolewa na benki hiyo.Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na benki hiyo. Meneja wa Benki ya Posta Tawi la Shinyanga Lawrence Munisi akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa kabla ya kukabidhi msaada uliotolewa na benki hiyo.
********
  Na Mwandishi Wetu 
BENKI ya Posta tawi la Shinyanga imetoa msaada wa mifuko ya saruji tani saba na nusu yenye thamani ya sh. milioni 3 kwa ajili ya waathirika wa mvua ya mawe katika Kijiji cha Mwakata wilaya ya Kahama. 

 Msaada huo umekabidhiwa jana na Meneja wa Tawi la Benki ya Posta, Shinyanga Lawrence Munisi kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa na Mkuu wa Wilaya ya Kahama, Benson Mpesya. Akikabidhi msaada huo Meneja wa Tawi la Benki ya Posta Shinyanga, Lawrence Munisi alisema Benki ya Posta imeguswa na tukio zima la maafa ya mafuriko na mvua ya mawe iliyoleta madhara kwa wananchi hivyo imeamua kuchangia msaada wa mifuko ya saruji isaidie kwa wananchi walioathirika na janga hilo.

 “Kwa niaba ya Benki ya Posta, tunatoa pole kwa wale wote waliokumbwa na maafa haya ya mafuriko, na kwa msaada huu wa mifuko ya saruji tunaamini inaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa sana waathirika wote,” alisema Munisi akikabidhi msaada huo. 

 Aidha kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kahama na Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa, Mpesya alitoa shukrani za dhati kwa niaba ya waathirika wote na kuziomba taasisi nyingine na hata watu wenye uwezo kuiga mfano wa Benki ya Posta. 

 “Kwa kweli tunashukuru sana kwa msaada huu mliotoa Benki ya Posta, na tunaamini msaada huu utasaidia sana katika kurudisha mazingira mazuri kwa wale wote waliopatwa na maafa haya...Tunaomba pia taasisi nyingine ziunge mkono, maana hili janga ni la Taifa na takribani watu wengi sana wamepoteza malazi na mahitaji yao mengine muhimu," alisema Mpesya. 

 Mvua kubwa ya mawe iliyoambatana na upepo mkali iliyonyesha hivi karibuni katika Kijiji cha Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga ilisababisha maafa ambako watu kadhaa walipoteza maisha na wengine kujeruhiwa. Nyumba kadhaa zilianguka na nyingine kuezuliwa paa kutokana na upepo mkali ambapo baadhi ya familia zimekosa makazi.
Posted by MROKI On Friday, March 20, 2015 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo