Nafasi Ya Matangazo

September 28, 2014



Na Fadher Kidev Blog
MSHAMBULIAJI Didier Kavumbagu ameifungia Azam mabao mawili na kuipa ushindi wa 2,mfululizo katika Ligi Kuu ya Tanzania bara.

Kavumbagu aliyejiunga na Azam msimu huu akitokea Yanga, amefikisha mabao manne katika mechi mbili za ligi ya msimu huu alizoichezea timu hiyo.

Katika mechi ya kwanza dhidi ya Polisi Moro,Kavumbagu alifunga mabao mawili katika ushindi wa 3-1, iliyoupata Azam.

Kavumbagu alifunga bao la kwanza katika dakika ya 39,akimalizia mpira uliopigwa na beki Shomari Kapombe na kurudi uwanjani ambao ulimkuta na kuukwamisha wavuni.

Ilimchukua dakika tano za kipindi cha pili Kavumbagu kuifungia Azam bao la pili na kuwaacha wapinzani wao Ruvu Shooting wanaofundishwa na kocha Tom Olaba wakianza vibaya msimu huu kwa kupoteza mechi zote mbili za awali ikiwemo ile ya kwanza dhidi ya Prisons.

Katika mechi hiyo washambulaji wa Ruvu Shooting walionekana kukosa kabisa mbinu za kuipita beki ya Azam angalau kupata bao moja Angalau mshambuliaji mpya wa timu hiyo Chagu Faustine dakika ya 25 alipata nafasi akiwa nje ya 18 lakini shuti lake halikuweza kulenga lango la Azam ambalo lilikuwa linalindwa na Aishi Manula.
Posted by MROKI On Sunday, September 28, 2014 No comments

0 comments:

Post a Comment

  • Facebook
  • Twitter
  • Youtube

Labels

Blog Archive

Nafasi Ya Matangazo